Waziri Mkuu Majaliwa - Tekelezeni kwa vitendo falsafa ya 4r za Rais Samia

Waziri Mkuu Majaliwa - Tekelezeni kwa vitendo falsafa ya 4r za Rais Samia

Screenshot_2024-09-08-10-48-20-1.png
 
Utawala wa Samia ungeboreka mno kama Raisi angemwacha Majaliwa awe huru., PM ahakikishiwe nafasi yake.

Majaliwa sio mpole, majaliwa sio mkali.
Majaliwa yupo too strict..Nchi ingesogea...

Tatizo la Raisi wetu hafurahii wateule wake waki perform na Kuwin public recognition....anahofia bure.

Jerry slaa alionyesh Ana kitu exceptional ndani wizara ya ardhi..Samia kamtoa.
 
MAONO YA KOMREDI KINGUNGE NGOMBALE MWIRU YANAVYOPUUZWA NA UTAWALA WA SASA


View: https://m.youtube.com/watch?v=bFQpjz1N4Tk

Kada mkongwe akiangalia hali ya kisiasa Tanzania kwa sasa anaiona ni ngumu, ni tete na vilevile ina utata pia tafrani ya sintofahamu ni kutokana na amri ya rais .... yeye rais si kijana lakini si mzee ila kitamaduni ukishakuwa rais basi wewe ni mzee... hivyo tunamuomba rais . ..tuzungumze naye ..... aitishe kikao .... komredi Kingunge Ngombale Mwiru .... akielezea suala kubwa ni kuepusha ....


Wazee wa chama cha CCM sasa imetosha, muibane serikali yenu iliyopo madarakani kwa kushindwa kuzuia wimbi la utekaji wa raia nchini Tanzania

1725798128217.png

Photo: mzee wa chama, rais mastaafu Jakaya Mrisho Kikwete.
 

06 September 2024​

SEMINA ELEKEZI KWA VIONGOZI WAANDAMIZI WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI 2024​


View: https://m.youtube.com/watch?v=jsMEnkMCoc4

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka maafisa waandamizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Tanzania na viongozi wa vyombo vya usalama wa Wizara hiyo kutekeleza kwa vitendo na kuiishi falsafa ya R NNE (4R) ya Rais Dk. Samia S. Hassan ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

View attachment 3089167
Amesema hayo leo Septemba 06, 2024 wakati alipofungua Semina elekezi kwa viongozi waandamizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Weruweru River Lodge, mkoani Kilimanjaro, Tanzania.

Amesema kuwa ni muhimu kuifahamu vyema falsafa hiyo ya Rais Dkt. Samia Hassan na kuitekeleza kwa vitendo. “Nina imani kubwa kwamba uongozi wa juu wa Wizara umeielewa vizuri falsafa hiyo, na semina hii elekezi ni ushahidi tosha wa kuitekeleza kwa vitendo”.


“Falsafa hii inajikita katika masuala ya Maridhiano (Reconciliation), Ustahamilivu (Resilience), Mageuzi (Reforms), na Kujenga upya Taifa (Rebuilding).

Hivyo, nitoe wito kwa washiriki ambao ni Maafisa Waandamizi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi pamoja na Menejimenti ya Wizara na Taasisi zake kuendelea kushiriki na kuishi kikamilifu falsafa hii,”amesema.
View attachment 3089154
Ameongeza kuwa semina elekezi hiyo ni sehemu muhimu kwa maendeleo ya kitaaluma na kitaasisi kwa maafisa waandamizi wa vyombo vya usalama, na husaidia katika kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kwa kufuata viwango vya kitaaluma na kisheria.

“Semina elekezi hutoa fursa kwa maafisa waandamizi kujifunza mbinu na taratibu mpya katika utendaji wa majukumu yao. Hii inajumuisha teknolojia mpya, mbinu bora za ulinzi na usalama, na mbinu za kisasa za kupambana na uhalifu,”.

Kwa Upande wake Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, engineer Hamad Masauni amemshukuru Rais Dk. Samia Hassan juu ya nia yake ya dhati kwa kufanya maboresho ya Wizara hiyo na vyombo vyake ikiwemo Jeshi la Polisi, Magereza, Uhamiaji na Zimamoto pamoja na Taasisi ya NIDA.
1000628878-1024x535.jpg

“Maboresho haya yanahusisha upandishaji vyeo wa kihistoria wa Maafisa, Wakaguzi na Askari wapatao 50,971 pia kuongeza Bajeti ya Miradi ya Maendeleo kutoka mwaka 2021/22 hadi 2024/25 ni Shilingi 262.2 ambayo ni sawa na asilimia 954.59 ya ongezeko la Bajeti ya Miradi ya Maendeleo,”amesema.

Amesema kuwa Ongezeko hilo la bajeti limesaidia kwa kiasi kikubwa kupatikana kwa vitendea kazi ikiwemo magari, mitambo, boti, vifaa vya TEHAMA na kadhalika

Falsafa zipi Mkuu kwa haya yanayoendelea ya utekaji na mauaji kila kukicha? Tunaenda wapi!!
 
Falsafa zipi Mkuu kwa haya yanayoendelea ya utekaji na mauaji kila kukicha? Tunaenda wapi!!

8 September 2024
Serikali ndiyo yenye dhamana kubwa ya kujibu hoja za wananchi kuhusu wimbi la utekaji


View: https://m.youtube.com/watch?v=xdd4HGlIZKc

Wakili wa kujitegemea na mwanaharakati wa kupigania haki za binadamu kutoka mkoani Mbeya wakili msomi Ezekiel Mwampaka, amesema Serikali ndiye yenye dhamana kubwa ya kujibu hoja za wananchi kuhusu hali ya nchi kughubikwa na wimbi la watu kupotea katika mazingira ya kutatanisha.
 
12 September 2024

Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Wakuu Waandamizi wa Jeshi la Polisi 2024


View: https://m.youtube.com/watch?v=5OPBbiE_dtI

Mgeni rasmi Naibu waziri mheshimiwa Daniel Baran Sillo (Mb.) akifungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Maafisa Wakuu Waandamizi wa Jeshi la Polisi leo Septemba 12,2024 unaofanyika mkoani Kilimanjaro Tanzania .

Ally Senga Gugu katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani , IGP C.M Wambura mkuu wa Jeshi la Polisi, mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro na wakuu wa polisi wastaafu ni miongoni mwa waliuhudhuria mkutano huo.

Naibu waziri Sillo anatoa salamu za Waziri wa mambo ya ndani ameshindwa kuhudhuria mkutano huo kutokana na kutingwa na shughuli maalum, hivyo naibu waziri kumuwakilisha katika mkutano huu wa Maofisa wakuu waandamizi wa Polisi (senior officers conference) mwaka huu 2024.

Maadili na nidhamu ni muhimu ili kuweza kuwa waadiĺifu katika utendaji mzuri wa kazi na kuweza kuwasimamia walio chini yao

Mwaka jana 2023 mheshimiwa rais akifungua mkutano kama huu katika ukumbi wa Oysterbay Officer Mess jijini Dar es Salaam alisisitiza ushirikiano na kuhudumia umma wa watanzania.

Makamanda na maofisi mwaka huu jeshi la Polisi linatimiza miaka 60 tangu kuanza kuanzishwa mara baada ya Jamhuri ya Muungano kuanzishwa mwaka 1964 ...


Toka maktaba
2023 4 September

Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama anafungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Maafisa Wakuu Waandamizi wa Jeshi la Polisi Jijini Dar es Salaam leo Septemba 04, 2023.

1726129339237.png

1726129595547.png




TOKA MAKTABA:

07 July 2024​

MHE. SILLO AHITIMISHA ZOEZI LA MAFUNZO YA UPANDISHWAJI VYEO CHUO CHA MAAFISA WA POLISI KIDATU​


1719903143.jpg


SILLO AHITIMISHA ZOEZI LA MAFUNZO YA UPANDISHWAJI VYEO CHUO CHA MAAFISA WA POLISI KIDATU
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Daniel Sillo (Mb), amehitimisha zoezi la Mafunzo ya upandishwaji vyeo ya Uongozi Mdogo kwa Cheo cha Sajini Meja (SM) na Sajini Taji (S/SGT) wa Polisi Kozi Na. 1/2023/2024 katika Chuo cha Maafisa wa Polisi Tanzania kilichopo Kidatu Mkoani Morogoro.

Akihutubia katika hafla hiyo Juni 28, 2024 Mhe. Sillo amesema kuwa, anatambua mafunzo yalikuwa ya muda mfupi lakini yenye mambo mengi muhimu yaliyofundishwa kwa njia ya nadharia na vitendo na mada zote zilifundishwa.

"Lengo ni moja tu kwamba mtakaporejea kwenye vituo vyenu vya kazi muweze kuwa mmepata ujuzi na mbinu za uongozi za kuwasaidia katika usimamizi wa majukumu ya kazi mtakayopangiwa. Ni vyema nichukue fursa hii kuwapongeza wakufunzi wote waliowezesha kukamilika kwa mafunzo haya kwa ufanisi kama ninavyojionea hapa, amesema nimeelezwa na Mkuu wa Chuo kuwa wakati wote wa mafunzo mmeonesha kuwa wenye nidhamu ya hali ya juu na mmejitolea kwa moyo wa dhati katika kushiriki kwenye vipindi vyote vya mafunzo bila kutegea vipindi" Alisema Mhe. Sillo

Pia amewataka wale wote ambao bado wanaendelea na vitendo vya ukiukwaji wa maadili waache mara moja na wabadilike kifikra ili waweze kuwatendea haki wananchi kwani dhamana waliyopewa katika nchi hii ni kubwa na vyeo hivyo viwasaidie katika kuwasimamia Askari wa chini ili nidhamu na uadilifu viimarike Jeshini katika kuepuka malalamiko hayo.

Mhe. Sillo pia amewaelekeza kuhakikisha wanadhibiti ajali za barabarani, Biashara Haramu za Dawa za Kulevya ambayo inaathiri afya ya vijana pamoja na kushughulikia kesi za unyanyasaji wa kijinsia na ukatili wa Wanawake na Watoto vikiwemo vitendo vya ukatili dhidi ya makundi maalum wakiwemo watu wenye ulemavu wa Ngozi (Albino).

"Kama kuna jambo linaniumiza sana ni ajali za Barabarani hapa nitoe rai kwa wadau wote wa usafirishaji Madereva, Watumiaji wa Barabara na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani tushirikiane kusimamia Sheria na kuzingatia alama za Barabarani zilizowekwa kwa mujibu wa Sheria"

Aidha, amemshukuru Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa na iliyotukuka anayofanya katika kuhakikisha nchi inakuwa salama muda wote ikiwa ni pamoja na kuliwezesha Jeshi la Polisi kwa kuwapandisha vyeo Askari katika ngazi mbalimbali sambamba na kutoa kibali cha ajira kwa Askari wapya.

"Nizidi kutilia mkazo kwenye jitihada anazozifanya IGP Camillus Wambura za kupeleka Wakaguzi wa Polisi hadi ngazi ya Kata/Shehia kwa kutambua umuhimu wa Wakaguzi wa Kata/Shehia nchi nzima kwa kuwapa motisha na kuwawekea mazingira mazuri ya kazi kama ambavyo Mhe. Mhandisi Hamad Masauni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi alivyokwisha anza kwa kuwatambua wanaofanya vizuri kila mwaka" Alisema

Awali katika taarifa yake Kamishna wa Polisi Operesheni na Mafunzo CP Awadhi Juma Haji aliishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa jinsi wanavyoliwezesha Jeshi la Polisi kwa kulipatia Vitendea kazi vya kutosha pamoja na Rasilimaliwatu.

Mhe. Mgeni Rasmi Kozi hii unayokwenda kuihitimisha hii leo Chuoni hapa ni miongoni mwa Kozi zilizokuwa zikiendelea katika vyuo vyetu vingine hapa Nchi ambapo inafanya jumla Askari 3464 ambao wamedhuria Mafunzo na kuhitimu katika ngazi mbalimbali

Source : MOHA
 
Jeshi la polisi linapatiwa mafunzo na semina elekezi kibao kwa ngazi zote kuanzia maafisa wakuu waandamizi wakuu hadi wale wa ngazi za chini kabisa.

Lakini hatuoni mabadiliko ya utendaji wa kazi nini tatizo? Watu wasiojulikana wanatekeleza mambo yao maovu bila kutiwa nguvuni, ni wapi wanakwama au kupata kigugumizi?

Nini sababu hiyi ya Jeshi la Polisi kushindwa kuwabaini, kuwafuatilia na kuwakamata watu wasiojulikana ?
 
Back
Top Bottom