Waziri Mkuu Majaliwa toka hadharani uwaombe radhi watanzania

Waziri Mkuu Majaliwa toka hadharani uwaombe radhi watanzania

msovero

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2019
Posts
929
Reaction score
1,764
Kwako Waziri Mkuu (PM), Majaliwa Kassim Majaliwa

Mwaka jana ukiwa bungeni ulitoa ahadi ya kuajiri walimu 16,000 mwaka wa fedha 2019/2020.

Mpaka sasa hakuna kilichofanyika na bunge karibuni linavunjwa mnarudi majimboni kujipanga na Uchaguzi Mkuu.

Mh. Kassim kama unavyojua UCHAGUZI ni mchezo wa pata potea unaweza kurudi ama usirudi mjengoni. Je unawaachaje vijana na ahadi yako ya ajira 16,000?

Ajira 16,000 ni ahadi hewa?

Mh. Kassim wewe ni kiongozi wa juu serikalini tena ni miongoni mwa wanaodhaniwa kuwa warithi wa Rais magufuli baada ya kumaliza muda wake.

Hivyo hutakiwi kujiingiza kwenye propaganda za kuwalaghai vijana kwa sababu Unajishushia hadhi yako na kupoteza uaminifu kwa watanzania. Mambo kama hayo unapaswa kuwaachia wasaidizi wako wa chini siyo wewe Mh. Kassim (Prime Minister)

Mh. Kassim Kama ile ahadi uliitoa kwa bahati mbaya, basi busara ikuongoze ujitokeze hadharani uwaombe msamaha watanzania kwa ahadi yako ya uongo uliyowahaidi.

Watanzania ni waungwana naamini ukiwaomba radhi nao watakusamehe.
 
Ahadi ni deni,asipoitekeleza hapa duniai basi iyo kauli yake ni yenye kuulizwa siku ya hesabu
inasikitisha kwakweli kwa nimujuavyo Mh. Kassim sikutarajia kama angekuja kujiingiza kwenye propaganda kama hizi
 
inasikitisha kwakweli kwa nimujuavyo Mh. Kassim sikutarajia kama angekuja kujiingiza kwenye propaganda kama hizi
Labda mpango ulikuwepo ila yule mzee mwingine akaupotezea huo mpango kwa kudirect funds kwenye vipaumbele vyake vya miundombinu n.k
 
Kama umemsikiliza vizuri Magufuli utakua umegundua kitu kuwa kuhusu suala la ajira ni ngumu mno kutoka kwa sababu kama mnavyo mjua Magufuli kitu kikiwa ndani ya uwezo wake huwa anatamka hapo hapo na utekelezaji unaanza mara moja lakini leo kashindwa.

Hapa nazungumzia leo kipindi alipo kuwa akiwasifia wale vijana wa jkt walio jenga hapo Ikulu ameshindwa kutoa ajira hapo hapo waajiriwa kama alivyo fanya kwa wale wa mwaka jana alizitamka pale pale jukwaani lakini leo kashindwa kabisaa na kuwahaidi mpaka wamalize ujenzi.

Jkt ina vijana wengi makambini angetoa ajira kwa hao walio jenga kisha waje wengine kumalizia ila kashindwa hizi ni dalili za kuwa ajira hakuna ila ni geresha tu. Hata hizo zilizo pitishwa juzi bungeni kwa mbwembwe hakuna hata moja pale itakayo tolewa.
 
Total ya ajira 42,000 usisahau kwenye sector zote

Tunawaangalia tu jamaa wanavyojichanganya.
Katika hili wameshakwama ukizingatia muda uliobaki ni mchache kuweza kutekeleza ajira 42,000. Hapa hamna jinsi tukubaliane tu kwamba tulihaidiwa ahadi hewa
 
Sasa tukija kulima huko kwenu, watoto wako watafundishwa na nani?
Au unataka waendelee kuwa wajinga(sio tusi) kama wewe.
nyie walimu sijui mna fail wapi? kwanza nyie ndiyo jeshi kubwa kabisa hapa Tz, lakini kama ajira zimekataa si mfikirie nje ya 'box' la kuajiriwa na majaliwa ili Maisha yasonge mbele, yaani frustration zenu mnataka mumshushie majaliwa? wakati mnajua kabisa 'jiwe' ndiyo mwenye maamuzi yoote?, yaani mmekosa plan b, c. d etc. za Maisha, binafsi nakosa Amani kabisa nikiona walimu wanalalama bila kuwa na mpango mkakati wa kutatua changamoto zao…...
 
Labda mpango ulikuwepo ila yule mzee mwingine akaupotezea huo mpango kwa kudirect funds kwenye vipaumbele vyake vya miundombinu n.k
Mmm!
Majaliwa ni waziri mkuu ndiye mtendaji mkuu wa shughuli zote serikalini kwahiyo sidhani kama angeweza kuongea mambo ambayo hakuwa well informed.
 
daaa kweli Maisha magumu duuu. kulikoni kumnanga majaliwa wa wtu wanazengo njooni huku choma cha nkola tulime pamba na mahindi tutatoka tuu………….
Hapa hatumnangi tunamkumbushia ahadi yake aliyotuhaidi watanzania mwaka jana bungeni kuhusu ajira 16,000. Kumkumbusha siyo kumnanga..Elewa
 
Kwako PM, majaliwa Kassim Majaliwa

Mwaka jana ukiwa bungeni ulitoa ahadi ya kuajiri walimu 16,000 mwaka wa fedha 2019/2020.

Mpaka sasa hakuna kilichofanyika na bunge karibuni linavunjwa mnarudi majimboni kujipanga na uchaguzi mkuu.

Mh. Kassim kama unavyojua UCHAGUZI ni mchezo wa pata potea unaweza kurudi ama usirudi mjengoni. Je unawaachaje vijana na ahadi yako ya ajira 16,000?

Ajira 16,000 ni ahadi hewa?

Mh. Kassim wewe ni kiongozi wa juu serikalini tena ni miongoni mwa wanaodhaniwa kuwa warithi wa Rais magufuri baada ya kumaliza muda wake. Hivyo hutakiwi kujiingiza kwenye propaganda za kuwalaghai vijana kwa sababu Unajishushia hadhi yako na kupoteza uaminifu kwa watanzania. Mambo kama hayo unapaswa kuwaachia wasaidizi wako wa chini siyo wewe Mh. Kassim(Prime Minister)

Mh. kassim Kama ile ahadi uliitoa kwa bahati mbaya, basi busara ikuongoze ujitokeze hadharani uwaombe msamaha watanzania kwa ahadi yako ya uongo uliyowahaidi.

Watanzania ni waungwana naamini ukiwaomba radhi nao watakusamehe.
Pia magufuri aliahidi ajira 1000 za madaktari,ila wamepunguzwa mpaka 300 ndo walioripoti vituoni
 
Hii ni Serikali ya Miundombinu! Siyo Serikali ya kuwazia Ajira na Ustawi wa maisha ya Watanzania walio wengi.

Na ndiyo maana hata hotuba zao zimejaa maneno mengi ya "Tumejenga......., Tumenunua............" Ukija kwenye suala la Ajira kwa Vijana, Maboresho ya mishahara kwa wafanyakazi, kuimarisha Kilimo cha Kisasa na chenye tija, nk ndipo utakutana na sarakasi za kila aina.
 
Back
Top Bottom