Waziri Mkuu Majaliwa, Vijijini hatuhitaji taa za barabarani, hii ni kejeli

Viji
Taa ni lazima popote,barabara kuu zote zinapita kwenye vijiji,mbali mbali.Taa zitakapokuwa zipo kwenye barabara kuu za Vijijini,wananchi watafanya biashara mpaka usiku,gari zinazopita usiku,watanunua bidhaa zao,uchumi wa vijiji utainuka.
Ji hivi ambavyo watoto wa shule wanakaa chini hawana madawati, kwenye madarasa yasiyo na sakafu au chini ya miti, kipaumbele ni kuweka taa barabarani?
 

Watanzania hawana jema

Unasahau kwamba hizo taa ni sehemu ya kuimarisha ulinzi wa eneo. Mnajua kulaumu tu
Mnajua kulalamika tu
 
Sisi tunahitaji mkuu ni vibaka na vibakuzi pekee ndo watakataa mradi kama huo
 
Mkuu unaambiwa TANESCO ndilo shirika pekee la umma linaloingizia serikali matrilioni ya fedha kila mwezi. Huwezi kuikataa fursa hiyo ya kuwekewa taa za barabarani.

Kama ni madawa na maji, basi yatatokana na vyanzo vingine. Ugonjwa wa UVIKO 19 si bado upo, na takwimu tunazipeleka WHO, basi mkopo nafuu ujao unaweza kuelekezwa huko.
 
Kuna vijitu vinavyo ishi mijini huko vinajiona vyewewe vinahaki ya kunufaika na keki ya Taifa kuliko waishiyo vijijini, nani kakwambia wa vijijini hawataki taa barabarani? Wamechoka kutumbukia mitaroni.
 
Dili la mtu hilo kama ile minyororo na mabomba ya dar
 
Ni jambo jema hizo ndo kazi za serikali kwa jamii, kukiwa na barabara nzuri vijijini na taa kutapunguza vibaka, wachawi na kufanya vijiji vichangamke usiku kufanya biashara na kazi kiasi cha wananchi kuweza kumudu kulipia huduma zitakazopelekwa na serikali kama maji, umeme, kutumia usafiri Ili kuchangia kodi na mambo mengine mazuri yatakayofanya vijiji vizalishe ajira kwa kujenga mpaka viwanda, kuongeza ajira zote zinazotokana na mahitaji ya watu waliobalika kutoka kuishi kama wanyama na kuishi kama watu wenye utu na maisha ya kisasa tofauti na Sasa watu wa vijijini wanarudisha sana nyuma maendeleo ya kuchangia ajira kwa kuishi maisha ya kizazi cha kale kisichotaka mafanikio Wala kujiletea huduma za msingi zinazozalisha ajira na kutegemea watu wanaoishi mjini ndo wazalishe ajira na mazingira Bora ya huduma za kisasa hivyo Waziri Mkuu kwa hilo la kupeleka hizo barabara na taa vijijini ni jambo jema sana likawakulupue huko vijijini watuzalishie ajira.
 
Vijiji vingi vya mkoa wa Rukwa vina taa angalau pale centers unless hujui umuhimu wa hizo taa.

Punguzeni ushamba taa sio anasa na umeme sio kwa wenye hela nyingi.
 
Ukipeleka miundombinu ya kisasa kijijini basi kijiji hakitaitwa tena kijiji bali mji, sasa wewe ndiye Stupid kwani unataka kijiji kiendelee kuwa kijiji ilhali unakiondolea sifa zinazofanya kiitwe kijiji !!!!.
Kwa hiyo taa ndio miundombinu ya kisasa ya kufanya kijiji kuwa Mji? Stupid
 
Reactions: Tui
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…