Waziri Mkuu Majaliwa, Wahudumu wa Ndege ya Precision Air wanasema Wao ndiyo Walifungua Mlango. Huyu Muokoaji ‘Majaliwa’ aliufungua upi?

Hiyo kamba aliifunga nani kwenye ndege?
 
Mentality za hivi ni za kipuuzi sana, kwahiyo hata Mama Samia kafunguliwa milango ya Baraka hatuwezi kuzuia licha ya kwamba serikali yake imefeli Kila kitu? Au hata mtu ukiwa na cheti feki au umetoa rushwa kupata promotion basi tukae kimya sababu tu ni "bahati" na "mlango wa mafanikio umefunguliwa"!!

Utakua mshirika wa Ministries sio bure
 
Mkuu relax machungu ya maisha usije kuyamalizia kwangu.
 
Ni hivi wakati wahudumu wanafungua mlango kwa ndani Majaliwa alikuwa kwa nje na aliwasaidia kuuvuta.

Dogo kasaidia sana katika juhudi za uokoaji
 
Mkuu relax machungu ya maisha usije kuyamalizia kwangu.
Sio machungu ila nyie ndio mnaturudisha nyuma sana. Unakuta jitu limeiba kura alafu unasema Mungu akipanga hakuna wa kuzuia.... Mara sijui ndio bahati yake... Mara sijui wakati wake wa kuketi na wakubwa umefika!! Sasa unajiuliza hivi Mungu anaweza kweli kutumia uongo kumpandisha mtu? Au Mungu anaweza ruhusu ajali na makumi kufa Ili "shujaa" Fulani aajiriwe?

Hizi mentality ni za washirika wa Gwajima au Mwamposa. Embu kuweni na objective reasoning sio Kila kitu kuweka Imani mbele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…