Waziri Mkuu: Mashitaka Yamekuwa Mengi, Tunaongeza Mahakama Zinazotembea

Waziri Mkuu: Mashitaka Yamekuwa Mengi, Tunaongeza Mahakama Zinazotembea

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
FQOKGvHXsAApEMO.jpg
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema ongezeko la mashitaka limekuwa kubwa na kuweka wazi kuwa hiyo inachangia Mahakama zilizopo kutokishi mahitaji ya kutoa huduma kwa wote wenye mahitaji, ndio maana Serikali imeweka mpango wa kuongeza Mahakama zinazotembea (mobile court).

Ameyasema hayo wakati wa Kipindi cha Maswali na Majibu leo Mei 12, 2022, Bungeni Jijini Dodoma.

“Mahakama hizo zinazotembea zinatakiwa kununuliwa kwa wingi ili ziende zikatoe huduma katika Wilaya zote hadi wananchi wa Vijijini wasitumie gharama kubwa ya nauli kwenda kupata haki zao za kisheria.

“Wizara ya Katiba na Sheria itatueleza mpango wake wa kuongeza mahakama zinazotembea, niwasiii Wabunge wapitishe bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria ili wanunue magari yatakayotumika,” – Waziri Mkuu
 
Ahsante sana Mhe. Waziri Mkuu kwa kauli hiyo, Hata hivyo Wananchi wa Wailaya Mpya ya Ubungo yenye Makao Makuu yake Kata ya Kibamba Hakuna mahakama ya WILAYA tangu WILAYA hiyo ianzishwe.

Hivyo wananchi wa Wilaya ya Ubungo ktk Mkoa wa DSM wanahitaji wajengewe Mahakama ya Wilaya ili kuondoa adha wanayo ipata hivi sasa na kwa kuzingatia wakazi ktk eneo hilo ni wengi sana.
 
Baba tatizo siyo mahakama kutembea au kukaa zilipo,tatizo kubwa ni kucheleweshwa kwa haki kwa makusudi ili mhusika ajiongeze
kwa kutoa mlungula. Na usipojiongeza usishangae hata kama kesi ilionyesha utashinda,mh.hakimu anaipindisha unashindwa
na wakati wa kusoma hukumu unaambiwa rufaa iko wazi.

Ukiwa mweppesi wa kukata tamaa unapoteza haki yako,na kama una uwezo wa kupambana haki yako unaenda kuipatia mbele kwa gharama kubwa zaidi,na yule hakimu aliyehukumu vibaya hapo mwanzoni hawajibishwi. Hili linawafanya wengi kuendelea na mtindo wao huo mbaya. Mtindo huu upo sana mahakama za mwanzo.

Jambo hili lisiposhughulikiwa kwa weredi,hata tungeanzisha mahakama za kutembea na helkopta bado kesi zitarundikana.
 
Kuliko gharama zote hizo nyie mungeturuhusu tu tumalizane huku huku kitaa ingekuwa poa sana
 
Back
Top Bottom