John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Waziri Mkuu mpya wa Pakistan, Shebaz Sharif amesema nchi yake inapendelea zaidi amani na uhusiano wa kushirikiana na India, mtazamo ulioonesha kuchaguliwa kwake huenda kukatoa nafasi mpya ya kuwepo maelewano ya kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili jirani zenye silaha za Nyuklia.
Katika ujumbe wake wa shukrani baada ya kupongezwa na Waziri Mkuu wa India, Sharif amesema Pakistan inataka kuyatatua kwa amani masuala ya mivutano iliyobakia ikiwemo suala la Jammu na Kashmir.
Amesema Pakistan imejitoa muhanga kupambana na ugaidi na suala hilo linafahamika vizuri kwa hivyo ni muhimu kutafuta amani na kuelekeza nguvu katika kujenga maendeleo ya kijamii na kiuchumi miongoni mwa watu wa nchi hizo.
Ujumbe wake huo umemfanya Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi kumpongeza akisema taifa lake linataka amani na uthabiti katika eneo hilo ili kuondoa ugaidi.
Sharif alichaguliwa kuwa Waziri Mkuu, Aprili 11, 2022 baada ya Imran Khan kuondolewa madarakani kupitia kura ya kutokuwa na imani nae iliyopitishwa na bunge.
Source: DW