Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye arejea CCM, alijiengua CHADEMA baada ya kuambiwa na Mbowe 'Sumu haionjwi kwa kuilamba'

Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye arejea CCM, alijiengua CHADEMA baada ya kuambiwa na Mbowe 'Sumu haionjwi kwa kuilamba'

2005 alikuwa upande wa Salim Amed Salim akapigwa chini akakosa hata uwaziri kwenye serikali ya Kikwete.

2015 akamfuata fisadi Lowassa akaangukia tena pua na kukosa hata ukuu wa mkoa.

2020 anarudia tena kosa lilelile la kwenda kuunga mkono udikteta unaofikia mwisho oktoba na kuangukia pua.

Anguko la Sumaye ni funzo kwa vijana wanaojifunza siasa.
Tuliokuwa tunamwita Ziro awamu ya tatu hatukukosea
 
Mkuu;
Sentensi yako ya kwanza kwenye thread imeonyesha huijua hata historia ya Sumaye katika siasa!

Mtu aliyekuwa Waziri Mkuu kwa miaka 10 ulitaka awe waziri tena kwenye serikali ya Awamu ya nne?
Aya! hata uwenyekiti wa bodi ya maziwa??
Au u vice chancellor vyuo vya kata
 
Ndio maana mimi huwa sipendi kwenda kusoma Havard
 
Tutasikia mengi mno kuhusu Sumaye, ila ndio hivyo tena " Sumu haijaribiwi kwa kuonjwa"
 
2005 alikuwa upande wa Salim Amed Salim akapigwa chini akakosa hata uwaziri kwenye serikali ya Kikwete.

2015 akamfuata fisadi Lowassa akaangukia tena pua na kukosa hata ukuu wa mkoa.

2020 anarudia tena kosa lilelile la kwenda kuunga mkono udikteta unaofikia mwisho oktoba na kuangukia pua.

Anguko la Sumaye ni funzo kwa vijana wanaojifunza siasa.
Hahahahaaaa wale jamaaa uwezo wao wa kiuongozi ni mdogo sana huyu ndiye alikuwa waziri mkuu imagine hii nchi angeifanyia nini?? Wanabebwa na mfumo tu wa CCM lakini hawana uwezo wa vigezo vya kutuongoza.
 
Ok waombe sasa wakurudishie mashamba yako yote waliyopora,mifugo, na hata haki zako za kushika ukurugenzi CRDB
 
Masharti ya Sumaye ya kujidhalilisha na kula matapishi yake na kukiuka viapo vya gizani na hadharani alivyojiapisha ni pamoja na kurejeshewa eneo lake la Mabwepande na shamba lake la Morogoro aliloporwa kwa sababu alihamia CHADEMA mwaka 2015, ikiwa kama hilo limeshindikana basi alipwe fidia kwa thamani ya sasa.

Hii ndio CCM ya sasa ambayo kuna Rais mmoja mstaafu ambaye amekuwa dalali wa mambo haya, haijulikani kama dalali huyu ambaye anafanya haya kama anapewa 10% au lah.
 
Masharti ya Sumaye ya kujidhalilisha na kula matapishi yake na kukiuka viapo vya gizani na hadharani alivyojiapisha ni pamoja na kurejeshewa eneo lake la Mabwepande na shamba lake la Morogoro aliloporwa kwa sababu alihamia Chadema mwaka 2015 , ikiwa kama hilo limeshindikana basi alipwe fidia kwa thamani ya sasa .

Hii ndio ccm ya sasa ambayo kuna rais mmoja mstaafu ambaye amekuwa dalali wa mambo haya , haijulikani kama dalali huyu ambaye anafanya haya kama anapewa 10% au lah .
Na hiyo fidia itatokana na kodi zetu au zitatoka mfuko wa CCM? kama ni kweli basi hii nchi inahitaji maombi ya kufunga na kuomba
 
Mmawia,
jamani acheni tu, wamenitesa mpaka nikashika adabu, wakawakataza CRDB kunichagua popote ili nikose tu posho,wakafaulu nikapigwa nje, nikaambiwa nitangaze sigombei kwa masilahi ya CRDB nikasimama nikasema.

Moyoni naumia tu,hawakuishia hapo wakaenda kule Basutu tulipokuwa tunalima ngano,wakachukua, hawakuishia hapo wakakimbilia Kibaha wakadai sijapaendeleza wakabeba. Mwisho wakaja kwenye kodi, bana kabisa, bana kabisa nikaona nakufa jamani.

Nikatafuta namna ya kurudi nikaona aibu. Bahati nzuri nilipokosa Uenyekiti wa mkoa cdm nikasema ni hapahapo nitaliamsha nipate kutoka.Jamani wamenitesa wamenitesa kuwa mwanachama chama kingine ndugu zangu ni balaa.

Sasa nawaheshimu sana kina Mbowe, Zitto, Piter, Lissu, Lema na wengine wengi huko ni mashujaa, mimi nimeshindwa ngoja nirudi labda watanionea huruma angalau kama mahesabu ya kodi yatapungua.

Maana hiyo kodi niliyopigwa mzee utasarender tu hata kama wewe ni jiwe, huna namna.Acha niende kimwili lakini kiroho sipo nao kabisa kwa sababu mwenzangu naye alirudi huko kwani mnamsikia tena,hakuna kitu huko lakini basi tu.
 
Back
Top Bottom