Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye arejea CCM, alijiengua CHADEMA baada ya kuambiwa na Mbowe 'Sumu haionjwi kwa kuilamba'

Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye arejea CCM, alijiengua CHADEMA baada ya kuambiwa na Mbowe 'Sumu haionjwi kwa kuilamba'

Erythrocyte, Uyo rais mstaaf ni mwizi na lengo lake ni wizi wake usiendelee kujulikana. Jk alionekana kuwa watofauti. Alienda mbali mpaka akataka kuleta katiba mpya amabayo ingebana na kuwajibisha maraisi wezi, madictator na wanyanganyi.

Alihakikisha anaweka diktator mwenzake ili aendelee kulala na mafaili yenye uvundo, uvunguni mwake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Erythrocyte,
Haya ndiyo ya kuwaeleza wananchi.

Ni rahisi sana kwa wananchi kuyaelewa, hasa baada ya kuwaona wabunge wao wakinunuliwa, itakuwaje vigumu wasiyaelewe mkiwaeleza kinagaubaga?

Erythro, siku zote nawaambia mmeleza damu sana, kwa sababu mnapewa fursa nyingi sana na ushahidi uliowazi, lakini vyote inakuwa vigumu kuvitumia ili viwasaidie.

Lowassa je, aliahidiwa nini; alishapewa? Mme wa binti bado anasota rumande!

Hakuomba asamehewe, au inasubiriwa wakati mwafaka, ili hilo lilete manufaa kwenye uchaguzi?

Nasubiri kumwona Lowassa akimpigia Kampeni mhusika.

Maajabu ya nchi hii hayana kikomo.
 
Wana mtandao,

Huyu mzee Wapinzani walimpokea wakati hakuwa material kwao, zile tambo za kusema anaenda kufundisha siasa makini kwa ajili ya maendeleo ya baadae ilikuwa uongo, yamkini wakati anaaacha siasa alisema hajiungi na chama chochote, ilikuwaje akatimukia CHADEMA.

CHADEMA ijifunze kutopokea makapi ambayo hayana uvumilivu. Ameweza kuwachambua vilivyo, sasa tegemeeni mabaya baada ya kuwachunguza, kumbuka alienda kusoma Harvard na kumaliza chuo.
 
😁😁 Huyo sumaye ni wakumuombea tu mungu amsaidie apumzike kwa amani wewe mtu waziri mkuu miaka kumi kipi kinamsumbua kama siyo matamaa, uzuri mungu fundi kamuumbua acha atulie sasa.
 
mgt software, Mlimpokea wenyewe mkamsafisha mkampigia deki lami mlivyo vilaza mkampa ujumbe kamati kuu anawasolola tu leo unatuuliza hapa jukwaani kuhusu mashamba nenda kamuulize Mmawia aliyekuwa mlinzi wa hayo mashamba!

Cc.Mmawia!
 
Hayo ni mawazo yako isipokuwa Sumaye alikuwa kazini!
Masharti ya Sumaye ya kujidhalilisha na kula matapishi yake na kukiuka viapo vya gizani na hadharani alivyojiapisha ni pamoja na kurejeshewa eneo lake la Mabwepande na shamba lake la Morogoro aliloporwa kwa sababu alihamia CHADEMA mwaka 2015, ikiwa kama hilo limeshindikana basi alipwe fidia kwa thamani ya sasa.

Hii ndio CCM ya sasa ambayo kuna Rais mmoja mstaafu ambaye amekuwa dalali wa mambo haya, haijulikani kama dalali huyu ambaye anafanya haya kama anapewa 10% au lah.
 
Na hiyo fidia itatokana na kodi zetu au zitatoka mfuko wa ccm?kama ni kweli basi hii nchi inahitaji maombi ya kufunga na kuomba
Kodi zetu ndio maana tunatishwa tusijuzwe chochote kinachoendelea kama mbuzi mnadani
 
Hii nchi tunahitaji ibada ya kuzamishwa kwenye mafuta aina ya Petrol kisha tubatizwe kwa moto!
 
Erythrocyte,
Uongo hata hamna soni. Kwani sumaye ana umuhimu gani hata chama kiende kinyume na misingi yake ili yeye arudi. Yeye ndio anakihitaji chama kuliko chama kinavyomuhitaji.

Juzi yule savimbi aliyeko kule sweeden kaandika kama uhakika makatibu waastasfu kinana na makamba wamekataa kuhojiwa na kubwanga manyanga chama. Kumbe uongo wa kutunga. Mtu wa ovyovyo kwelikweli hata aibu hana kwa kula mikate ya siagi ya mabeberu.
 
Uongo hata hamna soni. Kwani sumaye ana umuhimu gani hata chama kiende kinyume na misingi yake ili yeye arudi. Yeye ndio anakihitaji chama kuliko chama kinavyomuhitaji. Juzi yule savimbi aliyeko kule sweeden kaandika kama uhakika makatibu waastasfu kinana na makamba wamekataa kuhojiwa na kubwanga manyanga chama. Kumbe uongo wa kutunga. Mtu wa ovyovyo kwelikweli hata aibu hana kwa kula mikate ya siagi ya mabeberu.
Wewe ndo huoni huo umuhimu wake maana zaidi ya kupiga mapambio ya kusifu na kuabudu unajua nini zaidi?si ujinga tu ndo unakusumbua-wewe kitendo cha rais kuacha majukumu yake na kwenda kumpokea Lowasa unaelewa nini hapo hata kama unaakili kiduchu
 
Back
Top Bottom