PostGE2025 Waziri Mkuu Mwigulu: Mpango wa Bima ya Afya kwa wote kuanza Januari. Hakuna kushikilia maiti

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mwigulu Lameck Nchemba, amesema kuwa mpango wa bima ya afya kwa wote unatarajiwa kuzinduliwa kuanzia mwezi januari 2026, huku akizihimiza hospitali zote nchini kujiandaa kikamilifu kwa ajili ya utekelezaji wa mpango huo.

Ameyasema hayo leo desemba 17, 2025, wakati wa ziara yake mkoani songwe, alipofanya ukaguzi katika maeneo yaliyokumbwa na changamoto wakati wa maandamano ya oktoba 29, 2025.
 
Serikali ambayo sijaichagua haiweZi kuchukua pesa yangu
 
Ninatamani atumie uzito huo huo aliouna pale ndugu wa marehemu wanapozuiliwa kuzika wapendwa wao, autumie kutoa miili ya mo29 ili izikwe kwa heshima na ndugu zao.
 
Hizo ni porojo tu za kisiasa kama ilivyo siku zote. Wakitoa hizo bima zao watu watabaki nazo mapambo.

Utakuwa ukienda hospitalini unaambiwa ugonjwa wako haupo kwenye mpango wa bima hivyo utafute mamilioni ya pesa za kugharamia matibabu yako.

Mara nyingine utaambiwa hospitali haina vifaa au wataalam hivyo usafiri uende kwenye mikoa ya mbali au utaambiwa hizo dawa hazipo hivyo ukanunue kwenye maduka binafsi ya dawa kwa bei kubwa.

Hapo wanatafuta tu kupunguza hasira za watu kwa sababu wanafahamu vizuri sana kwamba hawana ridhaa yao ya kuwatawala. That's all.
 
waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mwigulu Lameck Nchemba, amesema kuwa mpango wa bima ya afya kwa wote unatarajiwa kuzinduliwa kuanzia mwezi januari 2026, huku akizihimiza hospitali zote nchini kujiandaa kikamilifu kwa ajili ya utekelezaji wa mpango huo.

Ameyasema hayo leo desemba 17, 2025, wakati wa ziara yake mkoani songwe, alipofanya ukaguzi katika maeneo yaliyokumbwa na changamoto wakati wa maandamano ya oktoba 29, 2025.
Yupo wapi? Mbeya? Mihemko ya kimpumu. Kapumuliwa! GDP ipi hiyo?
 
waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mwigulu Lameck Nchemba, amesema kuwa mpango wa bima ya afya kwa wote unatarajiwa kuzinduliwa kuanzia mwezi januari 2026, huku akizihimiza hospitali zote nchini kujiandaa kikamilifu kwa ajili ya utekelezaji wa mpango huo.

Ameyasema hayo leo desemba 17, 2025, wakati wa ziara yake mkoani songwe, alipofanya ukaguzi katika maeneo yaliyokumbwa na changamoto wakati wa maandamano ya oktoba 29, 2025.
Lazima mtu ajitoe ufahamu ili kupata kiki.

Mwijaku kqjitoa hadi...... kapata kiki hatari.

Huyu jamaa ni kesi ya madaktari wa fahamu ndo wanaweza kumsaidia
 
Back
Top Bottom