Mafyangula
JF-Expert Member
- Jan 16, 2025
- 557
- 1,039
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amekishutumu chama kimoja cha siasa nchini akidai kinatumika na maslahi ya nje kuvuruga amani na mwelekeo wa taifa, akisisitiza kuwa Tanzania haiwezi kuongozwa kwa rimoti kutoka nje ya mipaka yake.
Akizungumza na wananchi wa Uyole mkoani Mbeya wakati wa ziara yake ya kukagua miundombinu ya umma na mali binafsi zilizoathiriwa na vurugu za kabla, wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, Dkt. Nchemba amesema baadhi ya vyama vya siasa vilivyokuwa havina hata uwezo wa kujenga ofisi sasa vinaishi katika hoteli za kitalii kwa muda mrefu, hali inayozua maswali kuhusu vyanzo vya fedha wanazotumia na namna wanavyopanga kuzirudisha fedha hizo.