PostGE2025 Waziri Mkuu Mwigulu: Tanzania haiwezi kuongozwa kwa rimoti

PostGE2025 Waziri Mkuu Mwigulu: Tanzania haiwezi kuongozwa kwa rimoti

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amekishutumu chama kimoja cha siasa nchini akidai kinatumika na maslahi ya nje kuvuruga amani na mwelekeo wa taifa, akisisitiza kuwa Tanzania haiwezi kuongozwa kwa rimoti kutoka nje ya mipaka yake.

Akizungumza na wananchi wa Uyole mkoani Mbeya wakati wa ziara yake ya kukagua miundombinu ya umma na mali binafsi zilizoathiriwa na vurugu za kabla, wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, Dkt. Nchemba amesema baadhi ya vyama vya siasa vilivyokuwa havina hata uwezo wa kujenga ofisi sasa vinaishi katika hoteli za kitalii kwa muda mrefu, hali inayozua maswali kuhusu vyanzo vya fedha wanazotumia na namna wanavyopanga kuzirudisha fedha hizo.

Atamalizia umri wake akiwa gerezani mwacheni aendelee kuropoka, Hussein Mubaraka Sadam Bashiru Ghadafi walikuwa jeuli na dharau zaidi yake. Hana kawaida ya kujisomea huyu. Namuona Nchimbi anakaujanja kidogo anajaribu kujiweke pembeni kimtindo.. Ngoma ngumu hii mwacheni aendelee kujimwagia Petrol.
 
Back
Top Bottom