DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema kuwa uharibifu wa miundombinu iliyotokea siku na baada ya vurugu za Oktoba 29, 2025 unapaswa kuwa funzo kwa taifa, akibainisha kwamba miundombinu hiyo si mali ya serikali bali ni matokeo ya jasho, kodi na kujinyima kwa wananchi wote.
Akizungumza Jumatatu jijini Dar es Salaam katika ziara yake ya kutathmini athari za matukio hayo, Waziri Mkuu amesema Watanzania ndiyo wanaobeba gharama za ujenzi wa barabara, vituo vya afya, miundombinu ya maji, shule na huduma nyingine zote za umma.
Dkt. Mwigulu amesisitiza kuwa katika utaratibu wa mapato ya nchi, fedha zinazotumika kujenga miundombinu hutokana na kodi na michango ya wananchi hata pale inapoelezwa kuwa ni mradi wa serikali.
Waziri Mkuu amesema Watanzania hujikamua, hujinyima na hujibana ili kufanikisha miradi ya maendeleo. Kwa sababu hiyo, kitendo cha kuchoma, kubomoa au kuharibu miundombinu ni sawa na mtu kulichoma shamba lake mwenyewe.