Waziri Mkuu Mwigulu: Watanzania Tunzeni Akiba ya Chakula, Mvua zimechelewa

Waziri Mkuu Mwigulu: Watanzania Tunzeni Akiba ya Chakula, Mvua zimechelewa

Waziri Mkuu wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka Watanzania watunze akiba ya chakula walichonacho na waepuke matumizi yasiyofaa kutokana na hali ya kuchelewa kwa msimu wa mvua.

Waziri Mkuu ametoa wito huo leo jioni (Jumapili, Desemba 14, 2025) wakati akizungumza na baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya, ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma.

Amewaeleza viongozi hao kutoka mikoa ya Dodoma na Singida kwamba Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ilitoa utabiri wa mwelekeo wa msimu wa mvua za vuli na mvua za msimu kwa kipindi cha Oktoba 2025 hadi Desemba 2025 na kipindi cha mwezi Novemba, 2025 hadi Aprili 2026 mtawalia.

“Kutokana na utabiri huo, baadhi ya mikoa nchini inatarajiwa kuwa na mvua za chini ya wastani hadi wastani na kutawaliwa na vipindi virefu vya ukavu na mtawanyiko wa mvua usioridhisha,” amesema.

Source Jambo Tv

Mimi napenda CCM
 
Sio tutunze amani, amani ndio kila kitu bana🤣
 
Hivi mpango ya hazina ya chakula ya Taifa siku izi hakuna tena?
 
Hii ni vita ya kiuchumi, mabeberu hasa marekani na Europe wanatuonea wivu na milo yetu mitatu, wamefanya njama mvua zisinyeshe, Marekani anaionea wivu Tanzania baada ya uchumi wa Tanzania kuwa uchumi imara zaidi kuliko ule wa marekani, kwahiyo watanzania tuungane kupambana na Marekani, kama vipi lile jeshi imara la JWTZ tuliombe liivamie marekani kuwaonya juu ya njama zao na wivu wao kwa Tanzania, najua kwa jeshi imara JWTZ police itawachukua siku tatu tu kuisambaratisha marekani, hatuwezi kuwavumilia mabeberu wasitishe mvua kunyesha ilihali tunawatazama tu. WHO ARE THEY?
 
Yaani maisha ya Tanzania yanategemea mawingu ya mvua, this is too bad.
Nimesikitika sana. Nchi ambazo hazina mvua, zina maendeleo kuliko sisi nchi yenye mvua na rasilimali.

Viongozi tunaoamini watuwakilishe kuharakisha kasi ya maendeleo. Nao wana akili kama za kwetu wananchi za miaka ya 1900s.

Tuna mvua na rasilimali tele, lakini tunashindwa kuvitumia.
 
Sasa hivi utaona masheikh wa Bakwata wanasema tuombe dua inyeshe mvua.
Mungu anatu-Zoom tu,,

Katupa akili tunashindwa kuitumia,mtaani nilipo vishachimbwa visima kama vitatu juzi tu hapa,na tunapata maji safi kabisa,ghalama ni almost million Tano, tabu ya maji imepungua kiasi kwetu, ardhi yetu Mungu katujalia kuna maji mengi chini karibia Tanzania yote, M/mungu anatushangaa kumsumbua kumuomba mvua wakati maji yamejaa chini ya ardhi kibao,
Huku ukanda wetu MITA 40 tu maji kibao, hivi wabunge au madiwani wanashindwa kuchimba visima kwenye kata zao japo kwa uchache kuonyesha tu wanawajali wapiga kura wao.
Kwa serikali ndio kabisa hawashindwi kuacha kutegemea maji ya mito kwa asilimia kubwa ilhali wakati wa kiangazi miaka yote maji yanakuwa ya tabu, wachimbe tu visima vikubwa kama Iko cha huko sijui wapi ambacho kinatoa maji litres 70.milion
 
Hakika
 
Huyu mwigulu nadhani akifanya tathmini ya hotuba zake toka amepewa uPM atashangaa sana.

Tanzania kuilisha dunia

Wakulime msiuze chakula kutakuwa na njaa.

Serikali itauza akiba ili iende ikanunue kwa wakulima.

Hatutoboi.
 
Back
Top Bottom