Nimemsikia Mbunge Lucy Mayenga akiwaomba wabunge wenzake watafakari upya kuhusu mkataba wa DP World.
Wakati huo huo Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa amesema hawatapuuza maoni ya wananchi wanayotoa kuhusu huo mkataba.
Hii tafsiri yake nini, ni kuwa Wabunge na WM wamegundua kosa lao, kuwa hawakutafakari kabla ya kuupitisha na walidharau maoni ya wananchi, kwanini hawakutafakari na kwa nini walidharau kelele za wananchi, sababu kuna baadhi ya watu kwa propaganda zao na maslahi yao wametumika kuupotosha Umma na kulipotosha Bunge.
Hebu fikiria Mb kama Musukuma asiye na uelewa wowote wa mikataba ya kimataifa, na mwandishi wa habari kama Kitenge kwa vile tu walitembelea ofisi za DP World na kukuta komputa zimepangwa vizuri wakadhani ndio ufanisi wenyewe, watu kama hawa wana faida gani kwa bunge na taifa.
Ifikie mahali watu wa aina hii wakiwemo Wabunge, waandishi wa habari au mtu yeyote anayeeneza habari za kupotosha Umma kwenye jambo kubwa kama hili na kuiingiza nchi kwenye hasara kubwa wahesabiwe kama WAHAINI, hawaisaidii nchi hawamsaidii rais, wakati wowote wanaweza kununuliwa na mataifa ya nje kwa tamaa zao na kufanya propaganda za uongo na kiliingiza taifa kwenye machafuko makubwa.
Hongera Waziri Mkuu na Bunge kuanza kutambua kuwa kuna watu wanafanya propaganda za uongo kwenye huu mkataba, nilijua kukaa kwako kimya ulikuwa hupendezwi na watu wa aina hiyo.
Nakutakia wewe binafsi na Bunge muwe na tafakuri njema kwa maslahi mapana ya Taifa letu.