Waziri Mkuu na Bunge wanataka kutafakari nini wakati walipitisha kwa 100%

Mimi ninahasira sana na mibunge, niligundua wabunge wa ccm wanauwezo mdogo sana yaani ni hamnazo kabisaaaaa
 
Kila kitu kitaenda kama walivyopanga wala hakuna wa kuzuia DP world wasifanye yao!! Ni suala la muda tu...... loading
 
Rushwa ni mbaya, mtu akizoea rushwa inafika wakati anaipractice hadharani, yamewatokea puani hali ni tete, ila muda si mrefu utasikia wabunge wameigeuka serikali, na srikali itabadili upepo kisha wanachama watiifu wataandamana kumpongeza No 1
 
Wananchi walipuuzwa sidhani kama DPW walifahamu hilo, walijua bunge ndio kila kitu.
 
swala la kubinafsisha bandari yetu haliepukiki kama tunataka kusonga mbele cha muhimu ubinafshishaji huu uwe wa maslahi kwa pande zote mbili..ila kuliko kuwaachia wezi pale bandarini ni bora ibinafsishwe tu..
 
Hakuna mtu anayepinga uwekezaji wanachopinga watu ni terms za mkataba.
Natambua hilo, but CCM wakishapanga lao kuhusu mikataba elewa kuna interest humo! Kamwe hawakubali kubreak agreement!!
 
Rushwa ni mbaya, mtu akizoea rushwa inafika wakati anaipractice hadharani, yamewatokea puani hali ni tete, ila muda si mrefu utasikia wabunge wameigeuka serikali, na srikali itabadili upepo kisha wanachama watiifu wataandamana kumpongeza No 1
You might be right tengeneza tatizo litaue watu wakusifu, hata wao sio wajinga wanapima upepo usishangae kusikia mama amesikia kilio chenu sifa zikaenda kwake.
 
Ila ccm imetuchokaa!! Kweli suala nyeti kama hili wakaona musukuma ndio wa kutuelezea kweli!!!
 
Ifike mahala Bungeni Elimu izingatiwe,ikipendeza wenye elimu ya mambo ya sheria/uchumi ndio waingie. Hawa wa kujua kusoma na kuandika kisa wanajua kuongea wanalitia hasara Taifa.
Vipi kuhusu kada zingine ukiachana na Sheria na uchumi?
 
Wananchi walipuuzwa sidhani kama DPW walifahamu hilo, walijua bunge ndio kila kitu.
Usijidanganye kwamba DP World walikuwa hawafahamu. Wanafahamu vizuri tu ila waliamua kupuuza kwasababu wanawafahamu sisi watanganyika ni watu wajinga ambao tunafikiria kwa kutumia matumbo. Hivi unadhani ishu ya bandari ndiyo uwekezaji wa kwanza wa kifisadi kuwahi kufanywa na United Arab Emirates (UAE) hapa nchini ? Wamekuwepo hata tokea awamu ya nne chini ya Jakaya Kikwete.

Kama una kumbukumbu ndogo nikikumbushe basi, kipindi kile twiga wetu wanapandishwa ndege na kuibwa kiholela, zilikuwa ni ndege za jeshi la United Arab Emirates (UAE). Wakina Dr Slaa wanavyopiga kelele hawa waarabu walisikia vizuri tu na kuona jinsi gani serikali haijali na imejaa watu wenye tamaa. Haya yanafanyika Raisi Samia alikuwa waziri kule Ikulu, hivyo anachofanya ni kuendeleza ufisadi uleule ambao ulifanywa na mtangulizi wake.

Kuihadaa Tanganyika waarabu wanatumia silaha tatu kubwa ambazo ndiyo udhaifu mkuu wa Tanganyika (Tanganyika's Achilles Heel): GREED, RELIGION and THE FAULTY UNION. Mengine sitayasema leo, nasubiri wakati sahihi....
 
Natambua hilo, but CCM wakishapanga lao kuhusu mikataba elewa kuna interest humo! Kamwe hawakubali kubreak agreement!!

Ni CCM hiyo hiyo iliunga mkono mkataba wa Bagamoyo Port wakati wa JK na ni CCM hiyo hiyo iliunga mkono kusitisha mkataba wakati wa JPM.
 
Ifike mahala Bungeni Elimu izingatiwe,ikipendeza wenye elimu ya mambo ya sheria/uchumi ndio waingie. Hawa wa kujua kusoma na kuandika kisa wanajua kuongea wanalitia hasara Taifa.
Division one yoyote iwe ACSEE, CSEE au BA, MA, Phd etc
 
Ifike mahala Bungeni Elimu izingatiwe,ikipendeza wenye elimu ya mambo ya sheria/uchumi ndio waingie. Hawa wa kujua kusoma na kuandika kisa wanajua kuongea wanalitia hasara Taifa.
Niuzalendo tu na watu kuzingatia ubinafsi, otherwise bungeni wasominwapo wengitu.
 
Hivi unaweza kumtuma msukuma na darasa lake la saba aje kutoa ufafanuzi wa vipengele vya mkataba, tena kwenye media? hivi ngozi nyeusi huwa hatuko serious kwenye mambo ya msingi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…