Waziri mkuu Nchemba: Kama mkandarasi ametumia fedha kwingine kamata Passport yake

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mwigulu Lameck Nchemba amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Ahmed Abbas Ahmed kumuita mkandarasi aliyekua anajenga barabara ya Kitai-Ruanda na kumtaka aendelee na ujenzi wa barabara hiyo kwa haraka kwani alishakabidhiwa malipo yote ya awali ya kazi hiyo.

Dkt. Mwigulu ametoa agizo hilo leo Disemba 16, 2025 alipokuwa akizungumza kwenye msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Peramiho Jenista Mhagama uliofanyika Ruanda, Mbinga mkoani humo.

"mwelekeze kwamba fedha alishapokea afanye kazi ionekane na aendee na kazi kwa kasi inayotakiwa"

Dkt. Nchemba amemtaka Mkuu huyo wa mkoa kama ikitokea mkandarasi huyo ikaonekana ametumia fedha hizo kwenye mambo mengine, hati yake ya kusafiria izuiliwe mpaka atakapofanya kazi hiyo.

Aidha amemuagiza pia Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega kwenda eneo hilo kuangalia maendeleo ya kazi hiyo
 
Chezea vyote lakini sio Passport za nchi huru za Duniani. Magufuli alifanya hilo kosa kumnyang'anya mkadarasi wa India passport yake yaliyoipata tanzania ni majuto India ilifuta ununuzi wa mazao yote waliyokuwa wakiringa nayo wakulima, Mbaazi zilikuwa zinagawiwa bure
 
Back
Top Bottom