Waziri Mkuu, stendi ya Songea inawalipa wengi

Ahaa! Shukrani

Nimekuwa nikijiuliza Bukoba Municipal na Bukoba Rural, Moshi Municipal na Moshi Rural, Morogoro Municipal na Morogoro Rural ilikiwaje waweke administrative seats mbili na kutenga mipaka ya wilaya moja.

Naona dalili zilizotumika ni wingi wa watu na ukubwa wa eneo. Maana mfano, Bukoba (Municipal x Rural) ni sawa na Mkoa wa Dar es Salaam (Ukubwa wa Eneo), ukiangalia Bukoba Municipality ni radius ya 13.2 huku Municipality ikiingia kwa Rural mara 3 au 4.

Nimejifunza.
 
Kwahiyo nauli huku kwetu unaaga ndugu jamaa na marafiki kuwa una safari, sasa kama huko ni nauli yakumpfikisha mtu stendi, aisee ni mbali nitakubaliana na hiyo km20
Labda nikupe ushauli siku ukitaka kusafiri nenda alfajiri stend ya zamani hua kuna vigari vidodogo nauri 3000 mpaka 4000.
 
Unazungumzia jiji la watu karibu milioni saba.. kwa ulinganifu na mji wa watu laki tatu.. yaani ukiweka vizuri kata ya Manzese yenye ukubwa wa ekari 700 kuna watu zaidi ya mara mbili ya walioko songea manispaa.

Kuna haja gani ya kupanua huduma hivyo!?
 
Na sera yetu ya Makazi (Human Settlement policy) inasisitiza kuwa na miji compact.. kupunguza uharibifu wa mazingira.. administrative costs, infrastructure costs na eventually kuwapunguzia watu gharama za kuishi mijini... Ukiondoa transportation factor unamnufaisha yule mtu wa chini kabisa.

Wakurugenzi badala ya kutumia MASTER PLANS KUGIUIDE MIRADI YAO WANAENDESHWA NA KIU YA MAPATO, NA SIASA.. HATUWEZI KUFIKA...

Iringa wangelipa fidia waweke stand eneo la makaburi pale juu karibu na soko kungeufanya mji kuwa vibrant zaidi.. wanakimbilia igumbilo kuanzisha mji mpya wakati hata wa zamani haujakomaa
 
Wakurugenzi wanachikimbia ni kulipa fidia kubwa.. ambayo pia ina faida kubwa zaidi.
 
Oke, nimeelewa vizuri sasa.

Naona kuliweka hili sawa ni vyema miji ikapimwa au kupangwa upya. Hapa ni hospitali, stendi, soko, shule zitakuwa sehemu ABCDE hii ni open space, mji unaanzia H unaishia X.
 
Oke, nimeelewa vizuri sasa.

Naona kuliweka hili sawa ni vyema miji ikapimwa au kupangwa upya. Hapa ni hospitali, stendi, soko, shule zitakuwa sehemu ABCDE hii ni open space, mji unaanzia H unaishia X.
Ndivyo inapaswa kuwa..

Harusi zinaheshimu sana kamati, mpango na budget..

Ila kwenye issue sensitive kama kujenga mji, tunataka tu-freestyle ..unabaki unajiuliza how sane are we!? Fr
 
Ukifika utaelewa.
 
waziri yumo humu,atakuwa ameyaona malalamiko.ila wakati mwingine watendaji wachini ndo source ya matatizo mengi,Jambo la ku sort out within a day,litachukua miezi.this altitude should change jamani.then wakiwafainyia curling wanaanza kulaumu.
 
Oke, nimeelewa vizuri sasa.

Naona kuliweka hili sawa ni vyema miji ikapimwa au kupangwa upya. Hapa ni hospitali, stendi, soko, shule zitakuwa sehemu ABCDE hii ni open space, mji unaanzia H unaishia X.
makosa yalifanyika tangu mwanzo,miji mingi ya Tanzania ,ilianza kujengwa tu bila ya kuwa na master plan ya mji.changamoto ndo hiz tunaziona sasa.mfano jiji la mbeya aise ,plan ya mji iko shagalabagala,yaani vijumba vimepangana utazani viota vya ndege.

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Bahati mbaya hawajifunzi kutokana na makosa kwa kufanya masahihisho au kuanza muendelezo bora kunusuru hali duni. Asilimia 90 ya miji haikupangwa na inazidi kujongea katika mtiririko dhoofu.
 
Km20 zinafika na kama zitakuwa hazijafika itakuwa km17
 
Kilometa 20 nje ya mji!!! Huo si ukichaa kweli!!!
Ndio akili za maccm hizo zimeishia hapo,,Sumbawanga iko hvyo hvyo wenye mabasi hawajaenda

Yaani ukifika usiku had ukatoboe kwako ni zaidi ya 10,000 na ukitaka uwahi saa kumi Hadi ukafike stand si chini ya 5,000 sasa si upumbavu huu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…