Waziri Mkuu: Tumesitisha Sunday school na Madrasa, tulichoruhusu ni Ibada tu tena zifanyike kwa muda mfupi kisha waumini waondoke

hebu fungeni safari za kuingia na kutoka Dar, hivi mnataka mtuue wote ama? hivi mnacheza na Covid-19? mnafikiri na hii ni kama tume ya uchaguzi?
 
Muda utaongea soon watasitisha hata hizo ibada manake sioni kinachozuiwa hapo!!ibada ilipaswa zisimamishwe Ila kwasababu ya sadaka
 
Juzi Msumbiji Wabunge kwenye kikao walikaa umbali wa mita 6 kutoka kwa mmoja hadi mwingine,,, Ila baada ya kikao walikusanyika ili kuweza kupiga picha ya pamoja..

Akili waliyotumia wasumbiji ndio anayotumia Waziri,, hasa aliposema wakusanyike kwa ibada kwa muda mfupi,, sasa muda mfupi ni dakika ngapi.?? na huo muda mfupi utazuia maambukizi kivipi..?? kwani virusi vinachukua mda gani ili visambae..??

Viongozi wanaleta ukawaida usiokawaida
 
Uongozi wa kanisa ninapo sali nawashangaa sana. Hawataki kutekeleza maelekezo ya TEC na Vatcan.

Wanakwaya walishaambiwa waachane na kuimba kuimba kwenye kila kipengele lakini hawasikii.

Mapadre nao nawashangaa, akifikia sehemu ya "Bwana utuhurumie.." badala aanzishe fasta kuongea anawaangalia wanakwaya, wanakwaya nao, bila hiyana wanaanza kuimba, hivyo hivyo hadi kwenye utukufu, mwanakondoo na zaburi baada ya somo la kwanza wanakwaya wanaimba tu.

Mapadre wameelekezwa mahubiri yasizidi dakika 30, lakini ndio kwanzaaaaa, wanajimwaga tu hata lisaa lizima utadhani hakuna korona
Sang'udi
 
Ivi corona inahitaji ibada iwe dakika ngapi au corona inataka tuabudu masaa ma ngapi?
 
Twende twende twende.

Hii imeonyesha wazi kuwa dini faida yake ni kustaarabisha jamii tu.
They can't do far from that.

Watu wa dini wangekuwa wanaweza kufanya zaidi ya hilo wasingepangiwa ratiba

Safi sana. Tunaambiwa siku zote msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Huu ndio UKWELI
 
Je, Kwanini Mbowe anataka wa Dar tufungiwe ndani?

Analengo gani ?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ana malengo mazuri kua watu tusiendelee kuambukizana. Mh.Mbowe ana akili sana katika ili. Watu wakikaa ndani kwa wiki moja au mbili kuna uwezo mkubwa kwa kuzuia maambukizi.Pia Serikali ina pesa nyingi tu na chakula cha kuwapa wananchi.Je,wewe unaeshangilia mikusanyiko una malengo gani na nchi yetu?
 
Njaa ya sadaka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ibada ni ruksa tena kwa muda mfupi - Sasa mbona manabii wanakusanya halaiki ya wafuasi wao kila siku na "kuwaponya" Corona - Hii pia ni ruksa?
 
Point yangu iko wazi sana. Labda kama hujaielewa. Hatuwezi kuendeshwa kwa remote na Saudia au Italy. Kama tunafanya maamuzi au tunashauri maamuzi yafanyike basi iwe ni kwa sababu ya faida yake na sio kwa kuangalia Rome na Mecca as if wao walipewa vichwa vyenye akili sisi tukapewa maboga. Hicho ndio nakataa na nitaendelea kukikataa.
 
Kwamba ibada zikifanyika kwa muda mfupi ndio CORONA haiwezi kusambaa makanisani na msikitini

Waafrika tumelogwa na aliyetuloga amekufa!!! Hii inanikumbusha mkutano wa Viongozi wa Kiafrika uliofanyika huko Namibia ambako viti vya wajumbe wa mkutano vilipangwa mbali mbali to observe social distancing; sasa cha ajabu baada ya ule mkutano wote wakajikusanya ili kupiga picha!!!! Defeating the whole purpose of social distancing!!!
 
Huu ndio utabiri wangu kulingana na upepo unavyovuma, na kwamba swala la kusitisha Ibada kwa sasa ni swala la muda tu kabla maamuzi hayo hayajafikiwa.

Tukijitahidi sana ni wiki hii, ila kwa wiki jayo, sidhani, unless hakuna ongezeko la wagonjwa wengine jambo ambalo naliona ni gumu kulingana na mazingira yetu na jinsi tunavyoiachia utadhani Bongo ni kisiwa.

Mabaa na clubs nazo hazitaachwa.

Muda utasema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…