Pdidy
Platinum Member
- Nov 22, 2007
- 62,101
- 38,487
Waziri Mkuu goodmorning
Nimeona nianze kukupongeza kwa kazi nzuri ya kusikiliza malalamiko ya wananchi mkoani
Waziri Mkuu nimeona niseme haya
Pamoja na kazi nzuri unayofanya yale maagizo huwa mengi hayatekelezwi. Mimi nilikuwa mshabiki sana wa ziara za Majaliwa, kwa kweli kuna mambo alikutana nayo ya aibu mikoani watu wamepiga pesa za Wananchi, pesa za miradi ambayo umeona na umesema majuzi.
Aliporudi tena kama unavyosema na wewe utarudi tena akakutana na mauza haya haya yanaendelea na waliotajwa wapiga dili wapo na wanaendelea kuwapo. Serikali inatoa pesa za miradi lakini wanaofanya kazi hawalipwi..means wale Makandarasi wanatafuta 3rdparty wanafanya kazi na hawawamalizii pesa zao
Majuzi niliumia sana kuona mtu mmoja analalamika anadai laki 2 na ujenzi umeisha miaka miwili na pesa zimeshalipwa zote na bado Mkurugenzi wa Halamashauri yuko kazini. Sijui yule baba anadai toka 2022 milion 2.8 haisaidii wale ni wa kufyeka waondoke kabisa kwenye mfumo sio mambo ya kuhamishana toka Kinondoni nenda Ilala..wa Ilala aende Ubungo utakuwa unasikitika kila siku ziara zako
Mwisho kabisa naomba usisahauu kupita Dar es Salaam na watu wawe huru kabisa kutoa kero zao. Waziri Mkuu kuna malalamiko mengi sana hasa Kinondoni
Kuanzia Ardhi, Barabara, Maji, Hospitali na mengineyo yaani hii Wilaya kama imelaaniwa, Waziri Mkuu
Kule Manispaa na ardhi kuna watu wanajulikana wapiga dili wa hati za watu wanatajwa bado wapo na hata ukija utaambiwa na bado wataendelea kuwepo hii ni kuumiza wananchi na sio kutibu tatizo
Mungu ibariki Tanzania