TAARIFA KWA UMMA.
Kumekuwepo na habari zinazoenea kwa kasi mitandaoni ambapo mtu moja aliyefahamika kwa jina la Donald Trump, umri 71 kabila mmarekani, akitoa maneno yaliyojaa uchochezi hali inayoleta taharuki kwa umma wa Mexico na Canada. Jeshi la polisi linasikitishwa na maneno hayo yanayofarakanisha wananchi. Tayari uchunguzi wa suala hilo umeanza hivi punde na umefikia pazuri.
Tunatoa onyo kali kwa watu wengine kujiweka mbali na kauli za uchochezi ambapo jeshi la polisi halitasita kuchukua hatua kali za kisheria.