Waziri Mkuu wa China asisitiza utekelezaji wa sera za kutuliza uchumi

Waziri Mkuu wa China asisitiza utekelezaji wa sera za kutuliza uchumi

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang jana alisisitiza umuhimu wa kutekeleza sera za kutuliza uchumi na kuunga mkono masoko, ajira na maisha ya watu.

Bw. Li Keqiang aliyasema hayo kwenye mkutano wa baraza la serikali la China, na kuhimiza juhudi za kuhakikisha uchumi wa taifa unaendeshwa kwa kiwango kinachofaa.

Amesema kuwa, hatua mbalimbali zenye ufanisi zimetekelezwa kwa ajili ya kukabiliana na changamoto zisizotarajiwa ambazo zimeibuka mwaka huu. Amesisitiza kuwa, maendeleo ni jambo muhimu katika kutatua masuala yote ya China, ni lazima kutekeleza wazo la maendeleo mapya, kusawazisha kwa ufanisi udhibiti wa janga la COVID-19 na maendeleo ya kijamii na kiuchumi, na kutoa kipaumbele katika kutuliza ongezeko la uchumi.
 
Nyakati za mashaka pale kabwela/maskini akipanda hatua moja kwenda juu:...MAREKANI CHINA WANAWANYATIA-TIA-TIA KWA NYUMA: Marekani karata zako :-demokrasia,haki za binadamu na taiwan ambazo unazitumia kisiasa mchina anakusomaa vyema. WHEN CHINA RULES THE WORLD by martin jaques
 
Back
Top Bottom