Waziri mkuu wa DRC, Sylvestre Ilunga ajiuzulu

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Sylvestre Ilunga Ilunkamba amejiuzulu rasmi kama waziri mkuu wa Jamuhuri ya kisemokrasi ya Congo, na kuwasilisha barua yake kwa Rais Félix Tshisekedi.

Bw Ilunga, ambaye ni mshirika mkuu wa mtangulizi wa Rais Tshisekedi, Joseph Kabila, ameongoza baraza la mawaziri la serikali ya Muungano kwa miezi 15.

Hatahivyo wabunge walipitisha kura ya kutokuwa na Imani na serikali yakeJumatano wiki hii na akapewa saa 24 awe amejiuzulu.

Kujiuzulu kwake kunatoa fursa kwa Rais Tshisekedi ya kuwateua washirika wake kama mawaziri.

Hadi sasa, utendaji wa Bw Tshisekedi umekuwa ukidhibitiwa na, muungano alionao na Bw Kabila ambao uliafikiwa wakati alipoingia madarakani miaka miwili iliyopita.

Ushindi wake katika uchaguzi mwezi Disemba 2018 ulisifiwa kama wa kihistoria-ambapo kulikuwa na makabidhiano ya kwanza ya utawala kwa njia ya amani ambayo hayakuwahi kushuhudiwa katika historia ya miongo sita nchini humo.

Huu ndio mwisho wa muungano kati ya Bw Kabila na Bw Tshisekedi

1612008006527.png
 
Sitaki kuamini DRC imepiga hatua kiasi hiki kidiplomasia kuliko aliyekuwa mlinda amani na mwalimu wao Tanzania.
Unazungumzia kura ya kutokuwa na imani au kujiuzulu?

Kura ya kutokuwa na imani wabunge wa Tanzania walitaka kumpigia Mizengo Pinda, ikazimwa bungeni.

Tanzania Uwaziri Mkuu Nyerere alijiuzulu (Tanganyika), Sokoine alijiuzulu, Lowassa alijiuzulu.
 
Mkuu samahani, HIVI hali ya maisha mjini New York ipoje, namaanisha cost of living. Je naweza kuwa naishi nje ya Jiji la New York na nikaweza kufanya kazi nikawa nawahi kazini ontime?
 
Kwa mbali namuona KABILA anavyotafakari jinsi ya kufanya mapinduzi na kumuweka kibaraka wake maana hii ni kama dharau kwake
 
Mkuu samahani, HIVI hali ya maisha mjini New York ipoje, namaanisha cost of living. Je naweza kuwa naishi nje ya Jiji la New York na nikaweza kufanya kazi nikawa nawahi kazini ontime?

Muwe mnakwenda na wakati; siku hizi sio lazima uende ofisini kufanya kazi, unaweza kufanya kazi kutoka mahala popote ulipo!!! Huwezi amini kuwa kuna watu wameajiliwa New York lakini wanafanya kazi toka Mbeya!!! Huwezi kuamini because you are still living in the agrarian age!!!
 
Kwa sababu wewe unadhani kila kazi inaweza kufanywa kwa kifurushi cha Tigo mtandaoni!??? Hembu kakagulie miradi ya uwekezaji huko mitandaoni tuone?!
 
Hahaha, kazi nitakayo kuwa assigned ni maintenance Mechanics sasa sijui nitafanyika VP online
 
Unazungumzia kura ya kutokuwa na imani au kujiuzulu?

Kura ya kutokuwa na imani wabunge wa Tanzania walitaka kumpigia Mizengo Pinda, ikazimwa bungeni.

Tanzania Uwaziri Mkuu Nyerere alijiuzulu (Tanganyika), Sokoine alijiuzulu, Lowassa alijiuzulu.

Waling'atuka; hawakujiuzulu
 
Mkuu samahani, HIVI hali ya maisha mjini New York ipoje, namaanisha cost of living. Je naweza kuwa naishi nje ya Jiji la New York na nikaweza kufanya kazi nikawa nawahi kazini ontime?

😲😲
 
Back
Top Bottom