Waziri Mkuu wa Tanzania akutana na Shaka Hamdu Shaka bonanza la NMB, wakabidhiwa hundi ya TZS 600M

CM 1774858

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2021
Posts
5,621
Reaction score
5,029

Summary,

SHAKA ASHIRIKI MBIO ZA NMB
IMG-20221001-WA0142.jpg

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndg Shaka Hamdu Shaka leo Jumamosi tarehe 01 Oktoba, 2022 amekuwa sehemu ya mamia ya washiriki katika mbio za NMB zilizofanyika viwanja vya Leaders Kinondoni, Dar es Salaam.

Kauli mbiu katika mbio hizi ilikuwa 'Mwendo wa Upendo' zilizolenga kuchangisha fedha kwa ajili ya matibabu ya Fistula kwa wanawake wenye tatizo hilo kupitia CCBRT.

*Mgeni rasmi katika mbio hizi alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa ambapo amefanikisha kuchangishwa kwa shilingi millioni 600 kwa ajili matibabu ya wanawake wenye matatizo ya Fistula.

AIDHA, SHAKA HAMDU SHAKA ALIMAARUFU MR PUTINI AMESEMA,RAIS SAMIA AMEGUSA MAISHA YA
WANANCHI BIMA YA AFYA KWA WOTE,

Shaka asema mpango huo utakapokamilika wananchi waiunge mkono serikali katika hili Kwani nia yake ni njema Sana,
IMG-20221001-WA0255.jpg

Aidha Mr SHAKA ameipongeza NMB kuhamasisha jamii katika maendeleo endelevu,

IMG-20221001-WA0250.jpg

Anaendelea kasema,CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimempongeza Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kugusa maisha ya wananchi kupitia mpango wa "Bima ya afya kwa wote" kwa kuwa utawasaidia wengi kupata huduma za matibabu kwa uhakika.
IMG-20221001-WA0243.jpg

Aidha, ameipongeza benki ya NMB kwa kuendelea kushiriki masuala ya kijamii yakiwemo yanayoihusu afya ambayo ni muhimu kwa wananchi
ambao ni wateja wao,
IMG-20221001-WA0244.jpg

Pongezi hizo zimetolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka baada ya kukaribishwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, atoe salamu za Chama katika mbio zilizoandaliwa na NMB kwa ajili ya kuchangia matibabu ya wagonjwa wa Fistula, waliopo katika Hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam.
IMG-20221001-WA0256.jpg

Mheshimiwa Waziri Mkuu, kwa kutambua matibabu haya yana gharama kubwa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi Ibara ya 83 kifungu (e) inaelekeza katika kipindi cha miaka mitano, tutahakikisha kwamba tunaweza mazingira rafiki ya upatikanaji wa huduma hizi za afya. Nichukue fursa hii kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi kumpongeza kwa dhati kabisa Rais Samia Suluhu Hassan na serikali anayoiongoza kwa kuweka mpango madhubuti ya bima ya afya kwa wananchi wote.
IMG-20221001-WA0245.jpg

Alisema wakati NMB wakishiriki jitihada katika kuimarisha sekta ya afya kwa kukusanya sh. milioni 600, Rais Samia ameshaweka miundombinu ya kuhakikisha kwamba wananchi wote wanapata huduma hizo kupitia bima ya afya ili kupunguza makali ya upatikanaji wa huduma hizi.

"Ndugu zangu nataka niwahakikishie kuwa hamtajutia uamuzi wa kuiamini serikali ya Chama Cha Mapinduzi. Kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi niwaahidi kwamba Chama kitaendelea kuziunga mkono taasisi zote zinazounga mkono juhudi za maendeleo. Kazi ni moja na kazi inaendelea bila ya kurudi nyuma.

Alisema Ilani ya Uchaguzi ya CCM Ibara ya 83, imeelekeza kwamba ndani ya kipindi cha miaka mitano, serikali inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi itaimarisha huduma za afya kwa wananchi, ikiwa sambamba na ujenzi wa vituo vya afya, upatikanaji wa vifaa tiba na kuimarisha miundombinu ya maeneo ya kutolea huduma za afya, NMB hongereni sana kwa kuunga mkono jitihada za utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi.

AIPONGEZA NMB
Shaka aliipongeza benki ya NMB kwa namna ambavyo imeweka mipango na utaratibu wa kuishirikisha jamii katika masuala mbalimbali ya kijamii.
IMG-20221001-WA0147.jpg

"Kitendo cha kuandaa tukio hili kutafuta fedha kwa ajili ya changamoto inayowakabili baadhi ya kinamama nchini ni hatua kubwa na ya kupongeza sana.
IMG-20221001-WA0246.jpg

"Fistula imekuwa ikiwakosesha kujiamini na imekuwa ikiwakosesha furaha baadhi ya akinamama, huu leo ni ukombozi wa kurudisha heshima, kurudisha utu na kurudisha kujiamini kwa baadhi ya akinamama ambao wanapambana na changamoto hii.

=== ===
 
Nimekuja kusoma khii thread kwa kuona Waziri Mkuu wa Tanzania akutana na Putin, lakini sioni jambo lolote kuhusu hilo. Ulikuwa unakimbizwa, au ndio kibano cha tozo ulikuwa ukiandika haraka data zisiishe?
 
🤣🤣🤣

Sikiliza hiyo clip acha maneno maneno,
 
Bima ya afya!!!?

Mngetuambia KWANZA kwanini NHIF inakufa, Michango yetu ni Mingi Sana mule kabla ya HII ambayo hatulijui itakuwaje!!
 
Dah! kumbe Tanzania tumejiweka wazi ni wafuasi wa Putin, Waziri Mkuu anasema kwa furaha kabisa akimuita Katibu wa Itikadi na Uenezi Putin kwa mbwembwe..ahahahah
 
Nimekuja kusoma khii thread kwa kuona Waziri Mkuu wa Tanzania akutana na Putin, lakini sioni jambo lolote kuhusu hilo. Ulikuwa unakimbizwa, au ndio kibano cha tozo ulikuwa ukiandika haraka data zisiishe?
Na hii danganyadanganya inaenda mpaka kwenye kodi zetu,
 
Nimekuja kusoma khii thread kwa kuona Waziri Mkuu wa Tanzania akutana na Putin, lakini sioni jambo lolote kuhusu hilo. Ulikuwa unakimbizwa, au ndio kibano cha tozo ulikuwa ukiandika haraka data zisiishe?

Dah! kumbe Tanzania tumejiweka wazi ni wafuasi wa Putin, Waziri Mkuu anasema kwa furaha kabisa akimuita Katibu wa Itikadi na Uenezi Putin kwa mbwembwe..ahahahah
Putin Ni jina kama majini mengine, Ndio hapa TANZANIA hata OSAMA tunaye
 
View attachment 2374160
Summary,

SHAKA ASHIRIKI MBIO ZA NMB
View attachment 2374293
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndg Shaka Hamdu Shaka leo Jumamosi tarehe 01 Oktoba, 2022 amekuwa sehemu ya mamia ya washiriki katika mbio za NMB zilizofanyika viwanja vya Leaders Kinondoni, Dar es Salaam.

Kauli mbiu katika mbio hizi ilikuwa 'Mwendo wa Upendo' zilizolenga kuchangisha fedha kwa ajili ya matibabu ya Fistula kwa wanawake wenye tatizo hilo kupitia CCBRT.

*Mgeni rasmi katika mbio hizi alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa ambapo amefanikisha kuchangishwa kwa shilingi millioni 600 kwa ajili matibabu ya wanawake wenye matatizo ya Fistula.

AIDHA, SHAKA HAMDU SHAKA ALIMAARUFU MR PUTINI AMESEMA,RAIS SAMIA AMEGUSA MAISHA YA
WANANCHI BIMA YA AFYA KWA WOTE,

Shaka asema mpango huo utakapokamilika wananchi waiunge mkono serikali katika hili Kwani nia yake ni njema Sana,
View attachment 2374285
Aidha Mr SHAKA ameipongeza NMB kuhamasisha jamii katika maendeleo endelevu,

View attachment 2374286
Anaendelea kasema,CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimempongeza Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kugusa maisha ya wananchi kupitia mpango wa "Bima ya afya kwa wote" kwa kuwa utawasaidia wengi kupata huduma za matibabu kwa uhakika.
View attachment 2374287
Aidha, ameipongeza benki ya NMB kwa kuendelea kushiriki masuala ya kijamii yakiwemo yanayoihusu afya ambayo ni muhimu kwa wananchi
ambao ni wateja wao,
View attachment 2374288
Pongezi hizo zimetolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka baada ya kukaribishwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, atoe salamu za Chama katika mbio zilizoandaliwa na NMB kwa ajili ya kuchangia matibabu ya wagonjwa wa Fistula, waliopo katika Hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam.
View attachment 2374289
Mheshimiwa Waziri Mkuu, kwa kutambua matibabu haya yana gharama kubwa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi Ibara ya 83 kifungu (e) inaelekeza katika kipindi cha miaka mitano, tutahakikisha kwamba tunaweza mazingira rafiki ya upatikanaji wa huduma hizi za afya. Nichukue fursa hii kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi kumpongeza kwa dhati kabisa Rais Samia Suluhu Hassan na serikali anayoiongoza kwa kuweka mpango madhubuti ya bima ya afya kwa wananchi wote.
View attachment 2374290
Alisema wakati NMB wakishiriki jitihada katika kuimarisha sekta ya afya kwa kukusanya sh. milioni 600, Rais Samia ameshaweka miundombinu ya kuhakikisha kwamba wananchi wote wanapata huduma hizo kupitia bima ya afya ili kupunguza makali ya upatikanaji wa huduma hizi.

"Ndugu zangu nataka niwahakikishie kuwa hamtajutia uamuzi wa kuiamini serikali ya Chama Cha Mapinduzi. Kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi niwaahidi kwamba Chama kitaendelea kuziunga mkono taasisi zote zinazounga mkono juhudi za maendeleo. Kazi ni moja na kazi inaendelea bila ya kurudi nyuma.

Alisema Ilani ya Uchaguzi ya CCM Ibara ya 83, imeelekeza kwamba ndani ya kipindi cha miaka mitano, serikali inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi itaimarisha huduma za afya kwa wananchi, ikiwa sambamba na ujenzi wa vituo vya afya, upatikanaji wa vifaa tiba na kuimarisha miundombinu ya maeneo ya kutolea huduma za afya, NMB hongereni sana kwa kuunga mkono jitihada za utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi.

AIPONGEZA NMB
Shaka aliipongeza benki ya NMB kwa namna ambavyo imeweka mipango na utaratibu wa kuishirikisha jamii katika masuala mbalimbali ya kijamii.
View attachment 2374294
"Kitendo cha kuandaa tukio hili kutafuta fedha kwa ajili ya changamoto inayowakabili baadhi ya kinamama nchini ni hatua kubwa na ya kupongeza sana.
View attachment 2374295
"Fistula imekuwa ikiwakosesha kujiamini na imekuwa ikiwakosesha furaha baadhi ya akinamama, huu leo ni ukombozi wa kurudisha heshima, kurudisha utu na kurudisha kujiamini kwa baadhi ya akinamama ambao wanapambana na changamoto hii.

=== ===
Leo 01/10/2022 Jumanne????
 
Back
Top Bottom