Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer atangaza kupunguza misaada kutoka Uingereza kwenda nchi nyingine

Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer atangaza kupunguza misaada kutoka Uingereza kwenda nchi nyingine

Hayo magari Lc vx v8 hatuwezi kuacha kuyanunua. Yanalandana na hadhi ya viongozi wetu.

Viongozi wetu siyo wa kutumia mikokoteni kama Rumion, au passo au sijui vitz.. hapana haiwezekani kabisa.
wenye kutoa misaada hawataendelea kupenda kuona misaada yao inatumika kwa mambo ya kifahari, kununua magari ya bei kubwa wakati yapo ya bei ndogo
 
Wenzao wanapunguza matumizi. Huku wanaponda hela ya mlipa kodi bila aibu! Ma V8, misafara mikubwa, masherehe, maposho, masafari, hata hawajali matumizi ya hela ya raia!
Hawa wafadhali wametukosea sana walitakiwa wawe wamekata misaada toka 80s,tungekuwa tumeishajitambua,haya mamikataba ya ajabu ajabu eti mtu wa jangwani ndiye anahifadhi misitu yetu, hadi kichefuchefu.Sheria za kimila na sungusungu tU zimehifadhi misitu karne na Karne Bunge la 2cry halina uwezo huo hadi Mwarabu.
 
Wale wazee wa kitonga na tusiopenda kujitegemea mambo yanazidi kuwa magumu! Akili itakuja tu!

Starmer announces big cut to UK aid budget to boost defence spending​


Keir Starmer has announced drastic cuts to Britain’s international aid budget to help pay for a major increase in defence spending, amid fears over Donald Trump’s commitment to European security.

Tue 25 Feb 2025

starmer-planning-big-cuts-to-aid-budget-to-boost-defence-spending-say-sources

25 Feb, 2025 19:05

Mungu aendelee kuwabariki Wazungu.
Aamin
 
Kwahiyo alifanya nn? Alisitisha kuomba msaada? Alijitegemea 100%?
Nashangaa wanaosema jiwe aliacha kuomba na kukopa akatumia pesa ya ndani, wakati huo CAG alisema deni la taifa limeongezeka watu wanashindwa kujiuliza deni la taifa linaongezekaje na wakati anko anatuambia anatumia pesa ya ndani?
 
Kwa mwaka huu wa fedha, bajeti ya kununua magari ni Bilioni 800. Hayo lazima zitanunuliwa tu. Watu walilalamika bajeti kubwa ya magari lakini rais alitetea na kusema magari lazima yanunuliwe, whether mnataka ama hamtaki.

Hela ya matumizi yasio ya msingi zipo za kutosha, za maendeleo hakuna, tunasubiri za misaada ya watu wa Marekani na Ulaya.

Bajeti inatengwa, 70% ni matumizi ya kawaida, 30% za maendeleo. Hixo 30% kwa mwaka zinaweza kupelekwa 10 ama 15 tu ila kwenye matumizi, hutumika hata zaidi ya 70% iliyopangwa.
Serikali ya hovyo hii, hovyo kabisa
 
Nashangaa wanaosema jiwe aliacha kuomba na kukopa akatumia pesa ya ndani, wakati huo CAG alisema deni la taifa limeongezeka watu wanashindwa kujiuliza deni la taifa linaongezekaje na wakati anko anatuambia anatumia pesa ya ndani?
Bila evidence hii nayo ni porojo tu
 
wenye kutoa misaada hawataendelea kupenda kuona misaada yao inatumika kwa mambo ya kifahari, kununua magari ya bei kubwa wakati yapo ya bei ndogo
Hayo magari ya bei ndogo ndiyo size ya nyie walala hoi. Sasa unataka mimi waziri ambaye pia ni mbunge nitembelee vitz au passo au lile gari lililokaa kama kasongo sijui rumion kweli?
 
Magu alikuwa mbele ya muda sana...


Jamaa alikuwa kama TIME TRAVELLER...
Hakuwa na lolote,aliponyimwa pesa za millennium challenge mpaka abadili sheria ya 'habari',alifanya chapu kubadili sheria Ili apate pesa
 
Kuna miradi ya maji vijijini inayoendeshwa na UK-AID. Kwa maana hiyo inakwenda kusimama?

Kichekesho kiko hapa,
Mradi mmoja wa kisima unagharimu Tsh. Milioni 122 ila hivi vijiji tokea uhuru serikali ilishindwa peleka maji hadi UK-AID walivyojitokeza kuleta ukombozi

Gharama ya V8 moja la fisadi inaweza komboa vijiji vinne na shida ya maji ikabaki historia, ila kwakuwa sio kipaumbele chetu, acha tulie "UK amesitisha misaada"
Huu utaratibu ameuanzisha Babu na utakuwa ni utaratibu bora kabisa kwa wajukuu zetu na hata vitukuu miaka mingi inayokija Mungu mbariki Babu na wote wanaochota hekima zake.Sisi acha tuende lee kulala usingizini na siasa zetu za chawa na uchawa.N a zile za kujua kusoma na kuandika.
 
Back
Top Bottom