Waziri mkuu yupo sawa kuwashauri wahitimu wa degree kwenda Veta, Kiburi cha wahitimu kimesababisha wawe watu wasio na mbele wala nyuma mitaani

Kauli ya PM haijafafanuliwa vzr, sio kila mhitimu wa chuo kikuu,lazima aende veta,kuongeza ujuzi,
Mathalani, wakati namaliza chuo na shahada yangu ya umeme, electrical engineering, huwezi kuniambia tena niende veta kusoma umeme wa majumbani! Wakati hiyo ni topic tu katika engineering ya umeme! Waalimu wanaofundisha veta, umeme, wengi ni wahitimu wa diploma kutoka DIT(nalijua hili, classmate wangu wengi wapo pale), sasa MTU atoke DIT, na bachelor aende tena veta! LA msingi veta kusoma ni ni,
Wife wangu alimaliza degree ya sheria UD, miaka 7 kitaa bila kazi!akaenda VETA kusomea Mambo ya kupiga picha, video editing, sasa hv ni mwendo wa kupiga mapicha kwenye shughuri,
Mdogo wangu ni Engineer wa mitambo, kaajiliwa, ili kuongeza kipato ikabidi aende veta kusomea video production and editing, sasa hv anakampuni ya kupiga picha kwenye masherehe! Hiki ndio kitu alichomaanisha PM, wahitimu wa vyuo, wasizodolewe, wapewe mwongozo na vitu vya kujifunza, ni matusi ya nguoni, MTU kasoma miaka 6 u dokta, unamtaka aende veta kujifunza kuchoma mahindi!
Kuna vitu kama CCTV camera, fire alarm system, alarm system, kama unajua kizungu kidogo, hata kama hukuwahi kusoma physics, ulisoma luggage, kiswahili na Historia, unaweza kujifunza, ukapata certifacate, na ukapata ajira,
Kuna kuendesha mitambo kama crane, makaterpilllar ya kujenga barabara,au truck driving, MTU yeyote anaweza kujifunza, hata kama ameishia LA Saba, kwenye bomba LA mafuta, Tanga, walitafuta Sana vijana wa kuendesha mitambo, ikawa shida kuwapata, kozi yake ni gharama kidogo, milioni moja kwa wiki mbili,
Tusitumie matusi na kejeli kuwaongelea hawa vijana wa vyuo vikuu,sio kwamba wamejilisha matumaini ya kuajiliwa, ndani ya mwaka,ndinga Kali, mjengo, I phone, Hi you ni vitu vya kawaida, nchi yetu kukosa ajira za, maana, kwa, vijana, halikuletwa na Mungu, wala si ulemavu, ni Sera mbovu tu za ccm,
Kama hujawahi, kukaa campus, (UD, Udom, DIT,MIST, Arusha tech), hutawaelewa, hawa, madogo!
 
Mkishashiba chips huku mmekaa ofisini kwenye viajira vyenu vinavyowapa uhakika wa kula mwisho wa mwezi, mnaona jobless wote wenye digrii hawana akili Chujio
Shida ya ajira sio yako peke yako, usijitoe fahamu. Shida ya dunia nzima hata nchi zilizoendelea. Ungekuwa na skill yoyote ya maana ungetumia elimu yako uliyofadhiliwa na bodi ya mkopo hata kutafsiri filamu za kigeni kwa kisawhili ungepata hata kumi kuliko kufanya unaonewa kwa kukosa ajira
 
H
Hilo mkuu wamefanya wengi sana lakin kama itakuwa hivo anavosema pm nkwamba iwe kama kadesturi sasa je kila mtu akienda VETA skwamba mafundi watakuwa cheap na kunyanyaswa kama wasomi wanavofanyiwa leo kwenye taasis mbalombali?.

Pia huko VETA wanasoma bure? Anyway kila asiye na ajira atulize akili na aulinde moyo wake afanye lililo bora kwa akili yake mwenyewe.

Kama waliotunga mitaala wanawaona waliosoma kwa mfumo wa mitaala yao kwamb ni vichwa maji, itawazekanaje tena wauamini ushauri wao wa VETA,?. wanataka wakwame tena miaka ijayo ili wawaite tena hawana akili za kujiongeza?.
 
Wife wangu alimaliza degree ya sheria UD, miaka 7 kitaa bila kazi!akaenda VETA kusomea Mambo ya kupiga picha, video editing, sasa hv ni mwendo wa kupiga mapicha kwenye shughuri,
Ujuzi una umuhimu sana, Waziri mkuu hajakosea
 
Ni bora mijadala ya elimu ikafanyika mara kwa mara huko mashuleni na vyuoni kuona ni namna gani tutapata wahitimu bora wenye uwezo wa kuanzisha miradi yao badala ya kutegemea soko la kuajiriwa tu
 
Wahitimu hapa Tanzania ni kama bado hawajitambui kichwani, utakuta mtu kasoma na kamaliza Chuo ila kichwani hamna kitu zaidi ya baadhi ya mistarı waliyokariri kwenye baadhi ya vitabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…