JUAN MANUEL
JF-Expert Member
- Nov 26, 2010
- 7,808
- 16,972
Kauli ya PM haijafafanuliwa vzr, sio kila mhitimu wa chuo kikuu,lazima aende veta,kuongeza ujuzi,Don't Put All your Eggs in One Basket, Heri nusu shari kuliko shari kamili
Unakutana na kijana fresh outta chuo / college ana degree yake akiwa na mategemeo makubwa sanaaa !!
huko vyuoni wamedanganyana vitu vingi sana, Uhalisia wa Tanzania ni X wao wanapeana matumani tofauti kabisa Z.
Kijana anamaliza degree yake ana miaka 23 lakini unakuja kumkuta ana 30 hajapiga hatua, bado ana ndoto nyevu nyevu za kuja kuajiriwa, ubongo wake upo tuned kuona maisha yanapatikana kwenye ajira pekee, ndivyo mfumo wa elimu yetu unavyowaaminisha wanafunzi tangu wakiwa wadogo.
Uhalisia upo tofauti sanaaa, ajira zipo chache sanaaa, vyuo vinazidi kuwa vingi, wahitimu wanazidi kuwa wengi, amini usiamini 70 % ya ajira ili upate mpaka uwe na connection, nje ya hapo ni bahati au uwezo wako.
Ushauri wa Majaliwa ni mzuri lakini bado amewarembea vijana, mafunzo ya kujifunza kujitegemea kwa shughuli za kukuingizia kipato yaanze kabla mwanafunzi hajaingia degree.
Pindi akiwa chuoni siku za likizo, weekend, n.k. awe ana sehemu ya kwenda kujitolea kwa vitendo bure kabisa ikitokea kalipwa ni majaliwa, lengo ni kukusanya ujuzi na connections za wahusika wa shughuli hizo, hivi ni vitu ambavyo huwezi kuvipata kirahisi hata uwe na mtaji ndio maana wafanyabiashara wengi wanaoanza huwa wanafeli na kuangukia pua.
Hadi mtu anahitimu chuo awe ameziona changamoto za biashara kwa macho sio kusoma facebook, awe anavijua vibali, awe na namba na kufahamiana na wadau muhimu kwenye biashara, n.k.
Yote haya ni kumuandaa mhitimu ajiendeleze sio kuanza upya from scratch / zero, tena inapendeza zaidi akihitimu chuo analiunga huko huko mji au jiji alikosomea huku wakiwa na uwezo wa kujitegemea, hii ni faida sana kwasababu mambo ya kuanza kurudi vijijini au mikoani bila mishe ni jau, ndio mwanzo wa kutopata maendeleo yoyote zaidi mpaka unafika 30 upo vile vile ni sura tu imebadilika.
Panapotokea nafasi za ajira mtu awe ana uwezo wa kujilipia nauli, gesti, n.k. sio kuanza kusumbua tena wazazi , walezi, wajimba, n.k.
Mathalani, wakati namaliza chuo na shahada yangu ya umeme, electrical engineering, huwezi kuniambia tena niende veta kusoma umeme wa majumbani! Wakati hiyo ni topic tu katika engineering ya umeme! Waalimu wanaofundisha veta, umeme, wengi ni wahitimu wa diploma kutoka DIT(nalijua hili, classmate wangu wengi wapo pale), sasa MTU atoke DIT, na bachelor aende tena veta! LA msingi veta kusoma ni ni,
Wife wangu alimaliza degree ya sheria UD, miaka 7 kitaa bila kazi!akaenda VETA kusomea Mambo ya kupiga picha, video editing, sasa hv ni mwendo wa kupiga mapicha kwenye shughuri,
Mdogo wangu ni Engineer wa mitambo, kaajiliwa, ili kuongeza kipato ikabidi aende veta kusomea video production and editing, sasa hv anakampuni ya kupiga picha kwenye masherehe! Hiki ndio kitu alichomaanisha PM, wahitimu wa vyuo, wasizodolewe, wapewe mwongozo na vitu vya kujifunza, ni matusi ya nguoni, MTU kasoma miaka 6 u dokta, unamtaka aende veta kujifunza kuchoma mahindi!
Kuna vitu kama CCTV camera, fire alarm system, alarm system, kama unajua kizungu kidogo, hata kama hukuwahi kusoma physics, ulisoma luggage, kiswahili na Historia, unaweza kujifunza, ukapata certifacate, na ukapata ajira,
Kuna kuendesha mitambo kama crane, makaterpilllar ya kujenga barabara,au truck driving, MTU yeyote anaweza kujifunza, hata kama ameishia LA Saba, kwenye bomba LA mafuta, Tanga, walitafuta Sana vijana wa kuendesha mitambo, ikawa shida kuwapata, kozi yake ni gharama kidogo, milioni moja kwa wiki mbili,
Tusitumie matusi na kejeli kuwaongelea hawa vijana wa vyuo vikuu,sio kwamba wamejilisha matumaini ya kuajiliwa, ndani ya mwaka,ndinga Kali, mjengo, I phone, Hi you ni vitu vya kawaida, nchi yetu kukosa ajira za, maana, kwa, vijana, halikuletwa na Mungu, wala si ulemavu, ni Sera mbovu tu za ccm,
Kama hujawahi, kukaa campus, (UD, Udom, DIT,MIST, Arusha tech), hutawaelewa, hawa, madogo!