Waziri mkuu yupo sawa kuwashauri wahitimu wa degree kwenda Veta, Kiburi cha wahitimu kimesababisha wawe watu wasio na mbele wala nyuma mitaani

Waziri mkuu yupo sawa kuwashauri wahitimu wa degree kwenda Veta, Kiburi cha wahitimu kimesababisha wawe watu wasio na mbele wala nyuma mitaani

Don't Put All your Eggs in One Basket, Heri nusu shari kuliko shari kamili

Unakutana na kijana fresh outta chuo / college ana degree yake akiwa na mategemeo makubwa sanaaa !!

huko vyuoni wamedanganyana vitu vingi sana, Uhalisia wa Tanzania ni X wao wanapeana matumani tofauti kabisa Z.

Kijana anamaliza degree yake ana miaka 23 lakini unakuja kumkuta ana 30 hajapiga hatua, bado ana ndoto nyevu nyevu za kuja kuajiriwa, ubongo wake upo tuned kuona maisha yanapatikana kwenye ajira pekee, ndivyo mfumo wa elimu yetu unavyowaaminisha wanafunzi tangu wakiwa wadogo.

Uhalisia upo tofauti sanaaa, ajira zipo chache sanaaa, vyuo vinazidi kuwa vingi, wahitimu wanazidi kuwa wengi, amini usiamini 70 % ya ajira ili upate mpaka uwe na connection, nje ya hapo ni bahati au uwezo wako.

Ushauri wa Majaliwa ni mzuri lakini bado amewarembea vijana, mafunzo ya kujifunza kujitegemea kwa shughuli za kukuingizia kipato yaanze kabla mwanafunzi hajaingia degree.

Pindi akiwa chuoni siku za likizo, weekend, n.k. awe ana sehemu ya kwenda kujitolea kwa vitendo bure kabisa ikitokea kalipwa ni majaliwa, lengo ni kukusanya ujuzi na connections za wahusika wa shughuli hizo, hivi ni vitu ambavyo huwezi kuvipata kirahisi hata uwe na mtaji ndio maana wafanyabiashara wengi wanaoanza huwa wanafeli na kuangukia pua.

Hadi mtu anahitimu chuo awe ameziona changamoto za biashara kwa macho sio kusoma facebook, awe anavijua vibali, awe na namba na kufahamiana na wadau muhimu kwenye biashara, n.k.

Yote haya ni kumuandaa mhitimu ajiendeleze sio kuanza upya from scratch / zero, tena inapendeza zaidi akihitimu chuo analiunga huko huko mji au jiji alikosomea huku wakiwa na uwezo wa kujitegemea, hii ni faida sana kwasababu mambo ya kuanza kurudi vijijini au mikoani bila mishe ni jau, ndio mwanzo wa kutopata maendeleo yoyote zaidi mpaka unafika 30 upo vile vile ni sura tu imebadilika.

Panapotokea nafasi za ajira mtu awe ana uwezo wa kujilipia nauli, gesti, n.k. sio kuanza kusumbua tena wazazi , walezi, wajimba, n.k.
Kauli ya PM haijafafanuliwa vzr, sio kila mhitimu wa chuo kikuu,lazima aende veta,kuongeza ujuzi,
Mathalani, wakati namaliza chuo na shahada yangu ya umeme, electrical engineering, huwezi kuniambia tena niende veta kusoma umeme wa majumbani! Wakati hiyo ni topic tu katika engineering ya umeme! Waalimu wanaofundisha veta, umeme, wengi ni wahitimu wa diploma kutoka DIT(nalijua hili, classmate wangu wengi wapo pale), sasa MTU atoke DIT, na bachelor aende tena veta! LA msingi veta kusoma ni ni,
Wife wangu alimaliza degree ya sheria UD, miaka 7 kitaa bila kazi!akaenda VETA kusomea Mambo ya kupiga picha, video editing, sasa hv ni mwendo wa kupiga mapicha kwenye shughuri,
Mdogo wangu ni Engineer wa mitambo, kaajiliwa, ili kuongeza kipato ikabidi aende veta kusomea video production and editing, sasa hv anakampuni ya kupiga picha kwenye masherehe! Hiki ndio kitu alichomaanisha PM, wahitimu wa vyuo, wasizodolewe, wapewe mwongozo na vitu vya kujifunza, ni matusi ya nguoni, MTU kasoma miaka 6 u dokta, unamtaka aende veta kujifunza kuchoma mahindi!
Kuna vitu kama CCTV camera, fire alarm system, alarm system, kama unajua kizungu kidogo, hata kama hukuwahi kusoma physics, ulisoma luggage, kiswahili na Historia, unaweza kujifunza, ukapata certifacate, na ukapata ajira,
Kuna kuendesha mitambo kama crane, makaterpilllar ya kujenga barabara,au truck driving, MTU yeyote anaweza kujifunza, hata kama ameishia LA Saba, kwenye bomba LA mafuta, Tanga, walitafuta Sana vijana wa kuendesha mitambo, ikawa shida kuwapata, kozi yake ni gharama kidogo, milioni moja kwa wiki mbili,
Tusitumie matusi na kejeli kuwaongelea hawa vijana wa vyuo vikuu,sio kwamba wamejilisha matumaini ya kuajiliwa, ndani ya mwaka,ndinga Kali, mjengo, I phone, Hi you ni vitu vya kawaida, nchi yetu kukosa ajira za, maana, kwa, vijana, halikuletwa na Mungu, wala si ulemavu, ni Sera mbovu tu za ccm,
Kama hujawahi, kukaa campus, (UD, Udom, DIT,MIST, Arusha tech), hutawaelewa, hawa, madogo!
 
Mkishashiba chips huku mmekaa ofisini kwenye viajira vyenu vinavyowapa uhakika wa kula mwisho wa mwezi, mnaona jobless wote wenye digrii hawana akili Chujio
Shida ya ajira sio yako peke yako, usijitoe fahamu. Shida ya dunia nzima hata nchi zilizoendelea. Ungekuwa na skill yoyote ya maana ungetumia elimu yako uliyofadhiliwa na bodi ya mkopo hata kutafsiri filamu za kigeni kwa kisawhili ungepata hata kumi kuliko kufanya unaonewa kwa kukosa ajira
 
H
Baada ya kuhitimu elimu ya sekondari kabla ya kuendelea na elimu ya vyuo vya juu brother wangu alipendekeza nikapate mafunzo ya ufundi VETA kwanza ili niwe na ujuzi na stadi za kiufundi na mambo ya ujasiriamali pale Chang'ombe jijini Dar. Niliona brother na mke wake wamenidharau kunipeleka VETA nikachanganyike na vijana wa darasa la saba wakati mimi ni msomi mkubwa wa kusoma chuo kikuu, nilimkasikia sana brother kwa kuleta wazo la mimi kwenda VETA. Nilienda kwa shingo upande nikasoma fani niliyoichagua na kuhitimu vema kabla ya kuendelea na elimu ya juu na sasa najivunia kuwa nina elimu ya ufundi na elimu ya chuo kotekote nimepitia na nafiti ofisini na mitaani maisha yanaendelea bila kukosa shughuli za kufanya. Wasomi wa vyuo vikuu wakasome tu VETA ili wawe na option nyingi
Hilo mkuu wamefanya wengi sana lakin kama itakuwa hivo anavosema pm nkwamba iwe kama kadesturi sasa je kila mtu akienda VETA skwamba mafundi watakuwa cheap na kunyanyaswa kama wasomi wanavofanyiwa leo kwenye taasis mbalombali?.

Pia huko VETA wanasoma bure? Anyway kila asiye na ajira atulize akili na aulinde moyo wake afanye lililo bora kwa akili yake mwenyewe.

Kama waliotunga mitaala wanawaona waliosoma kwa mfumo wa mitaala yao kwamb ni vichwa maji, itawazekanaje tena wauamini ushauri wao wa VETA,?. wanataka wakwame tena miaka ijayo ili wawaite tena hawana akili za kujiongeza?.
 
Wife wangu alimaliza degree ya sheria UD, miaka 7 kitaa bila kazi!akaenda VETA kusomea Mambo ya kupiga picha, video editing, sasa hv ni mwendo wa kupiga mapicha kwenye shughuri,
Ujuzi una umuhimu sana, Waziri mkuu hajakosea
 
Ni bora mijadala ya elimu ikafanyika mara kwa mara huko mashuleni na vyuoni kuona ni namna gani tutapata wahitimu bora wenye uwezo wa kuanzisha miradi yao badala ya kutegemea soko la kuajiriwa tu
 
Wahitimu hapa Tanzania ni kama bado hawajitambui kichwani, utakuta mtu kasoma na kamaliza Chuo ila kichwani hamna kitu zaidi ya baadhi ya mistarı waliyokariri kwenye baadhi ya vitabu.
 
Back
Top Bottom