round kick
JF-Expert Member
- Feb 3, 2025
- 345
- 1,145
Don't Put All your hopes in One Basket, Heri nusu shari kuliko shari kamili
Unakutana na kijana fresh outta chuo / college ana degree yake akiwa na mategemeo makubwa sanaaa !!
huko vyuoni wamedanganyana vitu vingi sana, Uhalisia wa Tanzania ni X wao wanapeana matumani tofauti kabisa Z.
Kijana anamaliza degree yake ana miaka 23 lakini unakuja kumkuta ana 30 hajapiga hatua, bado ana ndoto nyevu nyevu za kuja kuajiriwa, ubongo wake upo tuned kuona maisha yanapatikana kwenye ajira pekee, ndivyo mfumo wa elimu yetu unavyowaaminisha wanafunzi tangu wakiwa wadogo.
Uhalisia upo tofauti sanaaa, ajira zipo chache sanaaa, vyuo vinazidi kuwa vingi, wahitimu wanazidi kuwa wengi, amini usiamini 70 % ya ajira ili upate mpaka uwe na connection, nje ya hapo ni bahati au uwezo wako.
Ushauri wa Majaliwa ni mzuri lakini ingependeza zaidi aseme vijana wapitie mafunzo kabla ya kuhitimu vyuo, jambo la pili sio lazima kwenda veta, mtu anaweza kwenda kujifunza kwa wataalam ambao tayari wapo site.
Pindi mwanafunzi akiwa chuoni siku za likizo, weekend, n.k. awe ana sehemu ya kwenda kujifunza kwa vitendo kwa kujitolea bure kabisa, ikitokea kalipwa ni majaliwa, lengo ni kukusanya ujuzi, maarifa na connections, hivi ni vitu ambavyo huwezi kuvipata kirahisi hata uwe na mtaji ndio maana wafanyabiashara wengi wanaoanza huwa wanafeli na kuangukia pua, ushahidi ni hawa hawa wahitimu wanapopewa mitaji wengi wanafeli.
Hadi mtu anahitimu chuo awe ameziona changamoto za biashara kwa macho sio kusoma facebook, awe anavijua vibali, awe na namba na kufahamiana na wadau muhimu kwenye biashara, n.k. akikusanya au akipewa mtaji anajiamini kwenye kitu anachoenda kufanya kwasababu ana ujuzi, maarifa na connections, sio kwenda facebook au kuomba ushauri humu jamii forums "nina shiling x nifanye biashara gani".
Yote haya ni kumuandaa mhitimu awe na uwezo wa kujitegemea baada ya kuhitimu chuo, tena inapendeza zaidi anapomaliza chuo aliunge huko huko mji au jiji alikosomea kuliko kuanza kurudi vijijini au mikoani kwao bila mishe anasubiria kuandika barua za kuomba kazi bila guarantee na ndio mwanzo wa kudorora na kupauka, mpaka anafika 30 hana mbele wala nyuma.
Panapotokea nafasi za ajira mhitimu awe ana uwezo wa kujilipia nauli, gesti, n.k. sio kuanza kukopa au kuanza kuomba, ni aibu sana inayokuongezea madeni na kukushushia heshima pindi unapokosa ajira tena na tena na tena.