Waziri Mkuu ziara zako mikoani hazitatui matatizo ya wananchi. Watumie viongozi mikoani

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
15,415
Reaction score
29,584
Huu ni upuuzi mwingine wa serikali ya awamu hii ya Raisi Samia eti Waziri Mkuu anazunguka mikoani kutatua matatizo ya wananchi. Waziri Mkuu anatakiwa kutatua matataizo katika ngazi ya kitaifa. Lakini ajabu ni kwamba Waziri Mkuu Mwigulu ameenda kutatua matatizo ya wananachi katika "individual level", yaani kibinafsi, wala sio ki-wilaya, walasio Kimkoa.

Kazi anayofanya Waziri Mkuu kwenye ziara hizi ni kazi inayopaswa kufanywa na Wakuu wa Wilaya, au hata wakuu wa mikoa kisha wampe taarifa. Waziri Mkuu anaposikiliza matatizo ya wananchi katika level ya mtu binafsi ni kupotezeana muda. Mwigulu anapotatua tatizo wa Mwanamalundi huko Mwanza inanisaidiaje mie Masudi hapa Dar es Salaam?

Waziri Mkuu anatakiwa asikilize matatizo ya Wananchi katika ngazi ya ki-wilaya au ki-mkoa - na ziara zake labda zingekuwa na maana zaidi kama angekuwa katika ziara zake anakutana na Wabunge, Wakurugenzi na Madiwani - na kutatua matatizo katika level ya maendeleo ya maeneo yao. Topiki zingekuwa issue za madaraja, maji, barabara, huduma za afya nk, akiongea na hao watu. Sio mambo ya kusema Kileo kamdhulumu kiwanja mjane fulani. Huko ni kutafuta umaarufu wa kisiasa.

Halafu Mwigulu atuambie. Hizi ziara zake zinagharimu kiasi gani? Tangu aanze ziara hizi zisizo na pua wala mdomo kusaidia wananchi katika individual context badala ya regional context, ametumia shilingi ngapi hadi sasa? Yeye na hao wanaoambatana nao, watakuwa wamelipwa mamilioni mangapi kuzunguka zunguka tu? Hizo tawala anazotembelea wametumia shilingi ngapi iliku-supprt ziara zake?

Haya ni matumizi mabaya sana ya fedha wa walipakodi. Hebu upuuzi huu ukome mara moja, na Waziri Mkuu arudi Dodoma kuendelea na majukumu yake ya kitaifa.
 
Mwigulu hajawahi kuwa kiongozi mzuri popote pale
Huyo anapokea rushwa cash kwenye sandarusi. Naweza kuthibitisha hili
 
Wenye matatizo wanapotatuliwa huwa na furaha na hufurahia ujio wa huyo kiongozi.

Kama haujawahi kuwa na matatzo, acha wenye matatzo watatuliwe.

Akae ofisi kwa nini? Mnataka akae ofsini ili mpate ajenda kuwa ni waziri wa kukaa ofisini?

Kwani hao watu hawajaona uwepo wa hao wakuu wa wilaya?

ACHA KILA MTU ATATULIWE MATATIZO YAKE KWA STAILI YAKE,
ACHA KILA KIONGOZI AONGOZE KWA STAILI ANAYOONA INAMFAA.
-ZAMU YENU YA KULETEWA TAARIFA OFISINI IKIFIKA MTAFANYA HIVO.

MBONA MNAWASHWA WASHWA, KWANI WALE WANAOTATULIWA MATATZO NYIE MNAUMIA? AU MNATAKA YAENDELEE KUWEPO MPATE AJENDA?

USHAURI: ITISHENI MKUTANO AU ANDAMANENI MUWAAMBIE WATANZANIA KUWA ZIARA ZA PM KUTATUA MATATZO SIYO HAKI NA NI KINYUME CHA DEMOKRASIA

MBONA MNA SPIDI KALI YA KUKOSA AJENDA?
 
Ziara za Mwigulu sioni kama zina tija kwa Taifa, maana anachokifanya ni kama anajijenga kisiasa tu. Nchi iko vipande vipande hata anachokifanya hata hakieleweki.

Tatizo la hawa viongozi wanajifanya wana akili nyingi kuliko hata wananchi wao kwa sababu tu wamekalia ofisi za umma kwa njia ambazo mpaka leo hazina baraka za wananchi.

Hizi ni fiction tu zinafanyika kujaribu kuwapumbaza wananchi na wananchi wenyewe hata hawawaelewi.
 
Mwigulu anajijenga mwenyewe kisiasa
Hapana, Mwigulu anajiharibu mwenyewe kisiasa.

Watakuwa kina Kikwete wamemwambia fanya ziara, hajui kuwa wanamuua kisiasa ili njia iwe nyeupe kwa mtu wao!
 
Ziara zake ni ishara tosha kwamba mifumo ya Tanzania na taasisi zake haija connect
 
Anaachaje per diem kaka? Watumishi wa umma kilio cha muda wote wapate safari sasa ntu kapata nafasi ya kujipangia mwenyewe kwa nini asizibe gaps na kumaliza madeni?
 
Wenye matatizo wanapotatuliwa huwa na furaha na hufurahia ujio wa huyo kiongozi.

Kama haujawahi kuwa na matatzo, acha wenye matatzo watatuliwe.

Akae ofisi kwa nini? Mnataka akae ofsini ili mpate ajenda kuwa ni waziri wa kukaa ofisini?

Kwani hao watu hawajaona uwepo wa hao wakuu wa wilaya?

ACHA KILA MTU ATATULIWE MATATIZO YAKE KWA STAILI YAKE,
ACHA KILA KIONGOZI AONGOZE KWA STAILI ANAYOONA INAMFAA.
-ZAMU YENU YA KULETEWA TAARIFA OFISINI IKIFIKA MTAFANYA HIVO.

MBONA MNAWASHWA WASHWA, KWANI WALE WANAOTATULIWA MATATZO NYIE MNAUMIA? AU MNATAKA YAENDELEE KUWEPO MPATE AJENDA?

USHAURI: ITISHENI MKUTANO AU ANDAMANENI MUWAAMBIE WATANZANIA KUWA ZIARA ZA PM KUTATUA MATATZO SIYO HAKI NA NI KINYUME CHA DEMOKRASIA

MBONA MNA SPIDI KALI YA KUKOSA AJENDA?
waambie hao wanataka mwisho wa siku waseme PM hawasikilizi wananchi kero zao..waache sindano iwaingie.
 
MH, DR WAZIRI MKUU WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MWIGULU LAMECK NCHEMBA ALICHOANZA NACHO KWASASA NI KIZURI MTOA MADA HEBU TULIA BADO MAPEMA.
 
Huu ni upuuzi mwingine wa serikali ya awamu hii ya Raisi Samia eti Waziri Mkuu anazunguka mikoani kutatua matatizo ya wananchi. Waziri Mkuu anatakiwa kutatua matataizo katika ngazi ya kitaifa. Lakini ajabu ni kwamba Waziri Mkuu Mwigulu ameenda kutatua matatizo ya wananachi katika "individual level", yaani kibinafsi, wala sio ki-wilaya, walasio Kimkoa.

Kazi anayofanya Waziri Mkuu kwenye ziara hizi ni kazi inayopaswa kufanywa na Wakuu wa Wilaya, au hata wakuu wa mikoa kisha wampe taarifa. Waziri Mkuu anaposikiliza matatizo ya wananchi katika level ya mtu binafsi ni kupotezeana muda. Mwigulu anapotatua tatizo wa Mwanamalundi huko Mwanza inanisaidiaje mie Masudi hapa Dar es Salaam?

Waziri Mkuu anatakiwa asikilize matatizo ya Wananchi katika ngazi ya ki-wilaya au ki-mkoa - na ziara zake labda zingekuwa na maana zaidi kama angekuwa katika ziara zake anakutana na Wabunge, Wakurugenzi na Madiwani - na kutatua matatizo katika level ya maendeleo ya maeneo yao. Topiki zingekuwa issue za madaraja, maji, barabara, huduma za afya nk, akiongea na hao watu. Sio mambo ya kusema Kileo kamdhulumu kiwanja mjane fulani. Huko ni kutafuta umaarufu wa kisiasa.

Halafu Mwigulu atuambie. Hizi ziara zake zinagharimu kiasi gani? Tangu aanze ziara hizi zisizo na pua wala mdomo kusaidia wananchi katika individual context badala ya regional context, ametumia shilingi ngapi hadi sasa? Yeye na hao wanaoambatana nao, watakuwa wamelipwa mamilioni mangapi kuzunguka zunguka tu? Hizo tawala anazotembelea wametumia shilingi ngapi iliku-supprt ziara zake?

Haya ni matumizi mabaya sana ya fedha wa walipakodi. Hebu upuuzi huu ukome mara moja, na Waziri Mkuu arudi Dodoma kuendelea na majukumu yake ya kitaifa.
Wala siendi mikoani au wilayani kutatua matatizo ya mtu au watu. Na ukiona nafanya hivyo ujue hapo nazuga tu lakini lengo la hizo safari zangu za kuzunguka mikoani ni kupiga mpunga (per diem).
We fikiria kila siku ijayo kwa Mungu nikiwa huko mikoani kuwazuga wajonga navuta kitu kama 2m.
 
Huu ni upuuzi mwingine wa serikali ya awamu hii ya Raisi Samia eti Waziri Mkuu anazunguka mikoani kutatua matatizo ya wananchi. Waziri Mkuu anatakiwa kutatua matataizo katika ngazi ya kitaifa. Lakini ajabu ni kwamba Waziri Mkuu Mwigulu ameenda kutatua matatizo ya wananachi katika "individual level", yaani kibinafsi, wala sio ki-wilaya, walasio Kimkoa.

Kazi anayofanya Waziri Mkuu kwenye ziara hizi ni kazi inayopaswa kufanywa na Wakuu wa Wilaya, au hata wakuu wa mikoa kisha wampe taarifa. Waziri Mkuu anaposikiliza matatizo ya wananchi katika level ya mtu binafsi ni kupotezeana muda. Mwigulu anapotatua tatizo wa Mwanamalundi huko Mwanza inanisaidiaje mie Masudi hapa Dar es Salaam?

Waziri Mkuu anatakiwa asikilize matatizo ya Wananchi katika ngazi ya ki-wilaya au ki-mkoa - na ziara zake labda zingekuwa na maana zaidi kama angekuwa katika ziara zake anakutana na Wabunge, Wakurugenzi na Madiwani - na kutatua matatizo katika level ya maendeleo ya maeneo yao. Topiki zingekuwa issue za madaraja, maji, barabara, huduma za afya nk, akiongea na hao watu. Sio mambo ya kusema Kileo kamdhulumu kiwanja mjane fulani. Huko ni kutafuta umaarufu wa kisiasa.

Halafu Mwigulu atuambie. Hizi ziara zake zinagharimu kiasi gani? Tangu aanze ziara hizi zisizo na pua wala mdomo kusaidia wananchi katika individual context badala ya regional context, ametumia shilingi ngapi hadi sasa? Yeye na hao wanaoambatana nao, watakuwa wamelipwa mamilioni mangapi kuzunguka zunguka tu? Hizo tawala anazotembelea wametumia shilingi ngapi iliku-supprt ziara zake?

Haya ni matumizi mabaya sana ya fedha wa walipakodi. Hebu upuuzi huu ukome mara moja, na Waziri Mkuu arudi Dodoma kuendelea na majukumu yake ya kitaifa.
Naunga mkono hoja.Inaonekana viongozi wote wa chama na Serikali hawatambui mamlaka yake.
 
Back
Top Bottom