Waziri Mpango umenena kuhusu Mamlaka ya Mapato Tanzania

Nimemsikiliza Waziri Mpango wakati akiongea na maafisa wa TRA nchini kuhusu kukusanya kodi na kufikia lengo la tr.2.

Nimependa na kuafiki kwa vile miradi mingi itakamilika kwa fedha ya ndani. Kitu ambacho amewaasa maafisa hao wazingatie ni kukusanya kodi kwa weledi, uaminifu na kwa hekima na busara ili kuifanya sekta binafsi kushamiri na ukusanyaji kodi kuwa endelevu.

Waziri alionya kuhusu kubambika kodi na kisha kuomba rushwa. Mimi ninakubaliana na waziri iwapo TRA hawatakuwa na njia rafiki za kukusanya kodi na kuwa wabunifu hawatafikia malengo hayo.

Rais aliwahi kuwaambia wapanue wigo wa kodi itozwe kwa watu wengi hata kama ni kidogo kidogo lakini kwa kupanua mzunguko wa ukusanyaji wake. (Kodi ya Tanzania inabebwa na idadi kubwa ya watu m. 56.)

Aidha wanapaswa kubadili mtizamo wao kwa wafanyabiashara wawachukulie kama washirika kibiashara na hivyo mitizamo ya kukomoa iachwe.

Pia kitengo cha elimu kitumike mno kuelemisha wafanya biashara na wananchi kwa ujumla badala ya kuvizia wafanye makosa na kisha kuwapiga faini zisizolipika. Hili litaua sekta ya biashara na kuikosesha serikali mapato endelevu. Mifumo ya teknolojia na elektroniki itumike zaidi katika ukusanyaji kodi.

Kuhusu tozo zipunguzwe viwango na idadi ili zilipike. Na hili lifanyike mapema mno. Itasaidia. Utaratibu wa sasa kutegemea faini na riba tu ni wa mpito si endelevu na itafika mahala utashindikana kwa vile wafanyabiashara watashindwa kulipa na kufunga biashara zao kwa vile ni makadirio nje ya faida- ni adhabu- na muda mwingi kuutumia mahakamani kwenye mashauri ya kodi.

Pamoja na wito na maelekezo ya waziri Kufikia malengo yasitafisriwe na maafisa wa TRA kama ni mapambano na kukomoa. Kamishna Mkuu ndg Mhede awe makini kwa kuwasimamia watendaji kwa karibu ili kufikia malengo bila kusababisha maumivu kwa wananchi na kuathiri biashara zao na hapo hapo kuchukua hatua kwa wala rushwa bila kuonea.

hili jambo halitowezekna kwa tz ytu! mpango wao bdo utakuwa palepale wa kodi nyang`anyi! hadi tuupite uchumi wa kati.. 🙄
 
TRA wanachofanyiwa ni sawa wanapelekwa Wodini wanazalishwa alafu wanalazimishwa wawe bikra
 
Mtu mmoja anawezaje kuwa na mamlaka ya kufunga biashara ya mtu at will wao wenyewe wanatengeneza mazingira ya kutengeneza miungu watu.

Mfanyabiashara anapopishana na afisa wa TRA kwenye kodi anayotakiwa kulipa hatua ya kwanza ni kutafuta afisa wa eneo lingine (independent) akakakugue na yeye aone kama atakuja na different opinion.

Assessment zake zikikubaliana na wa mwanzo mfanyabiashara kama bado aafiki swala linaenda kwenye mahakama za kodi or dispute resolution kama zipo.

Lakini kumwachia mtu mmoja awe na maamuzi ya kufunga biashara ya mtu huo ni upuuzi uliopindukia.

Wafanyabiashara nao wajifunze account ya biashara uwezi kuweka hela zako binafsi, kwenye kukaguliwa lazima watu wapate access ya account ya biashara for bank reconciliation purposes.

Management nzima ya TRA inabidi iangaliwe upya, kuna tatizo huko.
 
Hii ndiyo kero namba one Tanzania kufunga Account kienyeji kishamba kwa njia haramu za kishetani kwa nia ya kumkomoa mfanyabiashara ama kusaka Rushwa
 
Back
Top Bottom