Waziri mpya wa Mawasiliano, anza kazi na Azam Media. Wamepanga kutupiga kwenye vifurushi vipya

Waziri mpya wa Mawasiliano, anza kazi na Azam Media. Wamepanga kutupiga kwenye vifurushi vipya

BOB LUSE

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2014
Posts
3,738
Reaction score
3,199
Ndugu Mteja, kuanzia 1/8/24 kutakuwa na mabadiliko ya bei. Kifurushi cha 25000 kuwa 28000; 17000 kuwa 19000; 10000 kuwa 12000; 6000 kuwa 7000 na 3000 kuwa 4000.

Azam decoder hawana Ubora kuzidi Dstv, Wanatumia kigezo cha kutuonyesha mipira Ili kuchaji gharama zaidi, ongezeko hilo ni kama blackmailing, hakuna media nyingine wanaowapa ushindani kwenye mpira kwa Sasa. Ongezeko hilo sio halisia na maisha ya wananchi, ajabu Mzawa mwenzetu anatunyonya kuliko wageni wawekezaji.

Mmesubiri home boy apigwe chini ndio mlete ongezeko! Waziri nakusihi, liangalie kwa jicho la wananchi wanyonge..
 
Taarifa yao hii hapa

Screenshot_2024-07-24-10-06-56-1.png
 
Kwani Azam wanapata ruzuku serikalini? Hii ni biashara ya mtu binafsi na mfanya biashara yoyote lengo ni faida. Haya mambo hayamuhusu waziri wala serikali ni maamuzi ya kampuni binafsi hata sokoni tunaenda tunakutana na bei mpya lakini tunanunua. Kwa Azam kama huliwezi ni kuhamia sehemu unayoweza hakuna aliyelazimishwa kununua.
 
Back
Top Bottom