Waziri mpya wa Mawasiliano, anza kazi na Azam Media. Wamepanga kutupiga kwenye vifurushi vipya

Ikiwezekana ifike hata 50k angalau kama watanganyika wataelekeza mawazo kwenye mambo ya msingi yanayoihusu nchi, hii Simba na yanga imewapumbaza sana watu wengi.
 
Azam Media wameanza uwizi wa wazi wazi, yaani wanapandisha vifurushi vyao kiholela tena bila hata barua ya TCRA, wala TCRA kupitia madai yao ya kupandisha bei vifurushi vyao, huu ni wizi, TCRA inafaa wasimamishe hizo bei mpya hadi waangalie kama kuna haja ya kuongeza bei..!!
 
Package ya mpira ongezeko ni 3000 wakati package zisizo na mpira wameongezwa 1000.sijawahi ona ongezeko kubwa kiasi hicho, kwenye maisha haya magumu ya Bei za vitu kuwa juu
Basi kama ongezeko ni package zote hiyo sababu ya kurusha ligi ya Spain ni sababu haina maana
 
Badala umwambie aje kuung'oa mzizi wa matapeli wa mitandaoni

Inazungumzia kuhuau vifurushi
 
Azam wameleta VAR sasa wamepanga kutupandishia vifurushi vya ving'amuzi!

Hii si sawa bora wapate mpinzanj kwenye kuonesha ligi za nyumbani ili wasitunyanyase!
 
Azama ni kampuni binafsi, acha uboya.
 
Hivi nchi za wenzetu,ivi vitu ni gharama namna hii?? Vp na internet bundle??sema levels za maisha kwa apa bongo ni tofauti ukiwaza ulipe kodi ya nyumba,ulipie bills za umeme+maji,na vifurushi vya king'amuzi navyo kulipia😂😂
 
Nawashangaa wanaolalamika. At least ingekua ni tbc kweli.

Dawa yao ni kuacha kulipia, Wateja wote waweke mgomo baridi afu uone watavyomtesa bakhresa.
 
Watakwambia wameongeza Cheka Plus TV, Azam Sports 4 na kununua laliga kwa bei kubwa.
 
Nawashangaa wanaolalamika. At least ingekua ni tbc kweli.

Dawa yao ni kuacha kulipia, Wateja wote waweke mgomo baridi afu uone watavyomtesa bakhresa.
Mgomo kwenye entertainment??ur kidding right? Vitu vya starehe kama ivi unajisumbua bure😂
 
Kumbe umetoa maoni ukiwa hujui chochote kuhusu hayo maongezeko
Kwa nn usingeanza utafiti ndio uje kutoa maoni?
Nahitaji kujiridhisha tu lakini ukweli upo wazi azam anatoa matangazo kwa bei rahisi sana kulinganisha satellite service provider wengine. Kwasasa East and central Africa ameshika soko.
Unadhani watu wengine hawapendi kushika hili soko? Tatizo uwezo hamna.
 
Nahitaji kujiridhisha tu lakini ukweli upo wazi azam anatoa matangazo kwa bei rahisi sana kulinganisha satellite service provider wengine. Kwasasa East and central Africa ameshika soko.
Kulinganisha na kina nani? Hapa naamini umefanya research h yo utakuwa na majibu
Anatoa bei rahisi kulinganisha na wengine kina nani?
 
Kulinganisha na kina nani? Hapa naamini umefanya research h yo utakuwa na majibu
Anatoa bei rahisi kulinganisha na wengine kina nani?
Kwa hapa ndani ana competitors kama dstv , startimes , zuku n.k .zaidi ya dstv hakuna service provider mwengine hapo anaeweza kuwa programs alizonazo azam mshindani mkuu wake ni dstv ambaye watanzania wengi wameshindwa afford service unataka watu waende wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…