Waziri mpya wa Mawasiliano, anza kazi na Azam Media. Wamepanga kutupiga kwenye vifurushi vipya

Waziri mpya wa Mawasiliano, anza kazi na Azam Media. Wamepanga kutupiga kwenye vifurushi vipya

Niliamua kuendelea kwenda kibnda umiza kwa sababu azam tofauti na mpira wa bongo hamna Kingine cha maana chakuangalia
 
Sukari mbona wamepangiwa? serikali inaagiza sukari? acha ushamba, sasahivi kuna bidhaa muhimu duniani kama information? na ni haki no 1, kama hataki kupangiwa bei arudi kwao uarabuni akafanye biashara huko
Sukari? hivi wewe unajuwa sukari inaagizwa vipi? na uhakika hujui. Sasa turudi hiyo sukari ilapangiwa bei gani? acha wewe kuleta ujinga hapa. Mbaya umeanza kuleta chuki za kimaskini, ukiona mtu anaitwa watu kwa makabila ujuwe huyo maisha yamempiga kabaki kuwa mchawi. Arudi uarabuni wewe unajuwa wanachangia kiasi gani kwenye kodi nchi hii, wakati wewe nadhana hata TIN number huna unaongeza idadi ya watu tu nchi hii, unasindikiza watu.
 
Nadhani wako sawa kutokana na wakati wenyewe mbona gharama za vitu vyote zmepanda iweje wao washindwe kupandisha bei ya vifurushi? Halafu pia wanatarajia kurusha laliga na seria A
 
Dada angu sijui kama una akili timamu, Mtibwa sugar, TPC, Kagera sugar, Kilombero na Manyara sugar ni viwanda vya mumeo? kwa hiyo hawazalishi wanaagiza?
 
Nadhani wako sawa kutokana na wakati wenyewe mbona gharama za vitu vyote zmepanda iweje wao washindwe kupandisha bei ya vifurushi? Halafu pia wanatarajia kurusha laliga na seria A
Kwanini wapandishwe vyote? wangepandisha vinavyohusu mpira pekee
 
Dada angu sijui kama una akili timamu, Mtibwa sugar, TPC, Kagera sugar, Kilombero na Manyara sugar ni viwanda vya mumeo? kwa hiyo hawazalishi wanaagiza?
Ndio Dada yangu mdogo. Wewe nenda kajiongezee kidogo hujui hivi viwanda misaada wanayopata kwenye kuvisaidia kutopata ushindani wa nje ndio maana sukari zinaagizwa kwa special permint kutoka bodi ya sukari. Hujiulizi kwanini sukari tu vibali vyake ni nyeti sana vimeundiwa bodi ya sukari lakini sio mchele au mahindi? rudi darasani ukasome bi mkubwa ni ujinga kufananisha sukari na Azam.
 
Sukari mbona wamepangiwa? serikali inaagiza sukari? acha ushamba, sasahivi kuna bidhaa muhimu duniani kama information? na ni haki no 1, kama hataki kupangiwa bei arudi kwao uarabuni akafanye biashara huko
Kwahiyo serikali ndio inaagiza ving'amuz? Jinga kabisa
 
Ndugu Mteja, kuanzia 1/8/24 kutakuwa na mabadiliko ya bei. Kifurushi cha 25000 kuwa 28000; 17000 kuwa 19000; 10000 kuwa 12000; 6000 kuwa 7000 na 3000 kuwa 4000.

Azam decoder hawana Ubora kuzidi Dstv, Wanatumia kigezo cha kutuonyesha mipira Ili kuchaji gharama zaidi, ongezeko hilo ni kama blackmailing, hakuna media nyingine wanaowapa ushindani kwenye mpira kwa Sasa. Ongezeko hilo sio halisia na maisha ya wananchi, ajabu Mzawa mwenzetu anatunyonya kuliko wageni wawekezaji.

Mmesubiri home boy apigwe chini ndio mlete ongezeko! Waziri nakusihi, liangalie kwa jicho la wananchi wanyonge..
Homeboy lazima alikua kwenye huu mpango maana yeye alikua anatetea makampuni binafsi badala ya kuona wananchi hawanyonywi na wafanyabiashara wa mawasiliano.
 
Kwani Azam wanapata ruzuku serikalini? Hii ni biashara ya mtu binafsi na mfanya biashara yoyote lengo ni faida. Haya mambo hayamuhusu waziri wala serikali ni maamuzi ya kampuni binafsi hata sokoni tunaenda tunakutana na bei mpya lakini tunanunua. Kwa Azam kama huliwezi ni kuhamia sehemu unayoweza hakuna aliyelazimishwa kununua.
Sasa uhame Azam uende wapi kufuata unafuu
 
Wanaonesha La liga , serie A , Bundslesliga , France , baadhi ya match za Epl , afcon na ligi kibao bado mnataka kwa elfu 20 hivi watanzania nani kawaroga ? Na hapo ni full HD aah bana acheni hizo.
Swali langu, wamepandisha kwa package yenye hizo mipira au kwa package zote hadi ambazo hawana hiyo mipira?
 
Homeboy lazima alikua kwenye huu mpango maana yeye alikua anatetea makampuni binafsi badala ya kuona wananchi hawanyonywi na wafanyabiashara wa mawasiliano.
Naamini home boy alijua haya,haiwezekani tupewe notice ya wiki, Waziri asijue! Uzalendo haupo hapo
 
Swali langu, wamepandisha kwa package yenye hizo mipira au kwa package zote hadi ambazo hawana hiyo mipira?
Package ya mpira ongezeko ni 3000 wakati package zisizo na mpira wameongezwa 1000.sijawahi ona ongezeko kubwa kiasi hicho, kwenye maisha haya magumu ya Bei za vitu kuwa juu
 
Back
Top Bottom