Waziri mpya wa Mawasiliano, anza kazi na Azam Media. Wamepanga kutupiga kwenye vifurushi vipya

Waziri mpya wa Mawasiliano, anza kazi na Azam Media. Wamepanga kutupiga kwenye vifurushi vipya

Mwaka huu tena napokea ujumbe kuwa kuanzia tarehe 01/08/2024 kutakuwa na mabadiliko ya bei za vifurushi, hii ni baada ya mwaka jana kupandisha bei naona na mwaka huu pia wanakuja kivingine tena.

Ndugu Mteja, kuanzia 1/8/24 kutakuwa na mabadiliko ya bei. Kifurushi cha 25000 kuwa 28000; 17000 kuwa 19000; 10000 kuwa 12000; 6000 kuwa 7000; 3000 kuwa 4000; 500 kuwa 600; 1000 kuwa 1200.

Kwa hakika tutafika tumechoka sana
 
Mbona unalazimisha watu kwa fedha wanazo tafuta wenyewe, maana kama design unawakalipia kwa kutumia hela zao watakavyo.

Huyo DSTV anaenda kupotea polepole siku hizi kuna Router hizi,kwa 100k+ unapata speed ya kitosha link kibao za kucheck EPL,UEFA na ligi zote za ulaya.
 
Upo sawa kichwani kweli? Leo ukiuziwa saruji 100000 mfuko1 kwakuwa ni biashara ya mtu utaona ni Sawa? Nyie ndiyo majinga mliopo nchini. Serikali kazi yake ni ku regulate na ku control inflation ili wananchi wapate huduma kwa bei nafuu.
Kwanza unajuwa inflation nini? Unaweza kumpangia mtu nyumba akodishe kwa kodi kiasi gani? au ni Demand and supply kukiwa na mahitaji makubwa kuliko uwepo wa nyumba bei zitapanda. Unaenda sokoni nyanya unakuta bei moja kila siku? Serikali haifanyi regulate kwenye biashara za watu wanafanya kwenye mambo waliyotia mkono wao kama mafuta na nishati zingine lakini sio kwenye biashara za watu. Umeshawahi kufanya booking ya ndege au Hotel? Leo unaweza kukuta laki 2 jioni laki 3 hujiulizi kwanini?
 
Ndugu Mteja, kuanzia 1/8/24 kutakuwa na mabadiliko ya bei. Kifurushi cha 25000 kuwa 28000; 17000 kuwa 19000; 10000 kuwa 12000; 6000 kuwa 7000 na 3000 kuwa 4000.

Azam decoder hawana Ubora kuzidi Dstv, Wanatumia kigezo cha kutuonyesha mipira Ili kuchaji gharama zaidi, ongezeko hilo ni kama blackmailing, hakuna media nyingine wanaowapa ushindani kwenye mpira kwa Sasa. Ongezeko hilo sio halisia na maisha ya wananchi, ajabu Mzawa mwenzetu anatunyonya kuliko wageni wawekezaji.

Mmesubiri home boy apigwe chini ndio mlete ongezeko! Waziri nakusihi, liangalie kwa jicho la wananchi wanyonge..
Karine hii kulilia vifurushi vya TV ni ujinga sana, TV zimeachwa kwa jinga kutazama
 
Huyu jamaa mshamba,ila may be mtu wa marketing anatafuta masoko,ila anawakaribia watu nini cha kuangalia wakati fedha wanatafuta wenyewe.
 
Azam decoder hawana Ubora kuzidi Dstv, Wanatumia kigezo cha kutuonyesha mipira Ili kuchaji gharama zaidi, ongezeko hilo ni kama blackmailing, hakuna media nyingine wanaowapa ushindani kwenye mpira kwa Sasa
Hapa uko sahihi kabisa. Nape aliwapa Azam TV monopoly ya kuonesha mechi za mpira kinyume na sheria ya nchi na ya kimataifa ya fair competition katika biashara yo yote ile.

Waziri mpya wa habari awanyang'anye Azam TV hiyo monopoly ya mpira. TBC, ITV, Star TV, Clouds TV, Channel Ten, EATV etc nao waruhusiwe kuonesha hizo live football matches. Hapo lazima vifurushi vya Azam TV vitashuka automatically na jeuri hii ya Azam TV itakoma.

Hili lisipofanyika tutawaomba akina Madeleka, Mwambukusi na TLS kuwaburuza mahakamani Azam TV na Mwanasheria mkuu wa serikali kwa uvunjifu wa sheria hii ya kimataifa ya fair business competition.
 
TCRA waunde chombo cha ku-regulate bei ya TV za kulipia. Haya masuala mmiliki anaamka asubuhi na kutangaza bei mpya siyo kabisa.

Vv
 
Walivyosema wanaanzisha azam sport HD4 nikajua kabisa lazima bei ipande ila siyo mbaya mechi za ligi ya Tz, Bundesliga,League 1 na Laliga santander tutaziona
 
Screenshot_20240724_133607.jpg
wamepandisha na chaajabu hawataongeza hata channel
 
Hapa uko sahihi kabisa. Nape aliwapa Azam TV monopoly ya kuonesha mechi za mpira kinyume na sheria ya nchi na ya kimataifa ya fair competition katika biashara yo yote ile.

Waziri mpya wa habari awanyang'anye Azam TV hiyo monopoly ya mpira. TBC, ITV, Star TV, Clouds TV, Channel Ten, EATV etc nao waruhusiwe kuonesha hizo live football matches. Hapo lazima vifurushi vya Azam TV vitashuka automatically na jeuri hii ya Azam TV itakoma.

Hili lisipofanyika tutawaomba akina Madeleka, Mwambukusi na TLS kuwaburuza mahakamani Azam TV na Mwanasheria mkuu wa serikali kwa uvunjifu wa sheria hii ya kimataifa ya fair business competition.
Hao uliowataja wana uwezo wa kununua hizo mechi? Au unadhani ni bure
 
Back
Top Bottom