Waziri Mulamula: Watanzania walioko Ukraine wajitahidi waingie Poland. Wananchi msiwe na wasiwasi Serikali inafuatilia!

Habari ya vita mtu anaongea kama ananunua mitumba kariakoo.
 
MaChawa mna mapovu mengi sana.. povu lote hili kukataa ukweli . Pumbavu kabisa kabisa.
Ukweli ni kwamba viongozi wa MaCCM akili zao hazina akili.
Eti wajitahidi wafike POLAND kati kati ya vita, Shuwaieni sana.
 
Hapo ndio Kimbembe Sijui wana haligani Huko
 
Wakae tu huko huko, kwanza hao ni wanafunzi wakae hostel, tuongee na icrc uwezekano wa kuwapelekea msosi na medical logistics, tunao makomando pale ngerengere tuwatumie
 
Mbona nasisi tuko kwenye vita vya kutokomeza umasikini wakae tu huko, kuna dogo alikimbia Corona China akarudi Bongo anajuta
 
Hii ndiyo sababu kubwa ya serikali kukataa kutoa pasipoti kwa kila mwananchi. Serikali inajua raia wake wakipata matatizo kwenye nchi za watu, haina uwezo wa kuwasaidia.
 
Hatukutarajia kichaa cha Putin kingepanda kiasi hiki....tulidhani ni mikwara tu.
 
Waingie Poland kwa usafiri gani.

Hivi ukimwambia mtu aliyeko mtwara aingie Kenya bila msaada wa kumuwezesha kufika Namanga again ataingia kweli Kenya?

Watawezaje kufika huko na watakuwa wanakula nini?
Serikali ya akina mama. Hii nchi hii
 
Very low
Very unconcerned
 
Kwanini ilishindwa kuwatoa hali ilipoanza kuwa tete wakati wengine walipoanza kuondoka!

Tukumbuke vita haikuanza ghafla kwani maandalizi yalichukua zaidi ya wiki.
... intelejensia ilishindwa kung'amua uwezekano wa vita.
 
Wanabaguliwa! Wanaambiwa watembee kwa miguu magari hayatoshi kwa wa'ukraine' wenyewe! Jifunzeni kwa mataifa ya wengine kama China wamewezaje kuwaondoa raia wao zaidi ya 4000!
 
Alichokiongea waziri Mulamula hakina maana wala msaada
Heri angekaa kimya tuu

Mungu wanusuru binadamu wasio na hatia

Mungu watembelee rais wa Russia na Ukraine ukawape moyo wa suluhu badala ya kumwaga damu zisizo na hatia
Angekuwepo Magu haya yasingetokea maana Mulano asingekuwa mambo ya nje na ndege zote za air Tz zingeandamanishwa kwenda kuwachukua watz na WA Africa wanaonyanyapaliwa Ukraine! RIP mwamba raise wetu tuliyekupenda na kutupenda!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…