Waziri Mulamula: Watanzania walioko Ukraine wajitahidi waingie Poland. Wananchi msiwe na wasiwasi Serikali inafuatilia!

Waziri Mulamula: Watanzania walioko Ukraine wajitahidi waingie Poland. Wananchi msiwe na wasiwasi Serikali inafuatilia!

Waziri wa Mambo ya nje Mh Mulamula amewataka watanzania takribani 300 walioko Ukraine wajitahidi waweze kuingia Poland ambako uratibu unafanyika.

Mulamula amesema ameona ubaguzi unaoendelea Ukraine kupitia mitandaoni na amesikitishwa sana lakini wananchi wasiwe na wasiwasi kwa sababu serikali inafuatilia kwa karibu sana.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
Habari ya vita mtu anaongea kama ananunua mitumba kariakoo.
 
Acha utoto. CCM ndo nini. Wale watoto walioko kule wamepelekwa na CCM. Unaingiza Siasa kwa mambo serious. Umejiuliza kwanini wazazi hawakuwatoa watoto wao mapema? Kusoma Ukraine [emoji1255] Nchi maskini lazima mzazi ajiweze. Je Tanzania Ina Ubalozi Ukraine au inategemea Huyu wa Ujerumani? Mambo haya sio rahisi sana. Wengi wanaenda nje bila kujisajiri kwenye Balozi husika au kujitambulisha tu. Shida ikitokea ndo Serikali mnaikumbuka. Ikifanya jambo lazima mtafute lawama. Umeambiwa Sasa wanafanya utaratibu wao wafike tu Poland. Unakuja na Vyama. Wewe chama gani mkuu. Fanya tofauti.
MaChawa mna mapovu mengi sana.. povu lote hili kukataa ukweli . Pumbavu kabisa kabisa.
Ukweli ni kwamba viongozi wa MaCCM akili zao hazina akili.
Eti wajitahidi wafike POLAND kati kati ya vita, Shuwaieni sana.
 
Wakae tu huko huko, kwanza hao ni wanafunzi wakae hostel, tuongee na icrc uwezekano wa kuwapelekea msosi na medical logistics, tunao makomando pale ngerengere tuwatumie
 
Mbona nasisi tuko kwenye vita vya kutokomeza umasikini wakae tu huko, kuna dogo alikimbia Corona China akarudi Bongo anajuta
 
Hii ndiyo sababu kubwa ya serikali kukataa kutoa pasipoti kwa kila mwananchi. Serikali inajua raia wake wakipata matatizo kwenye nchi za watu, haina uwezo wa kuwasaidia.
 
Et wana nchi wasiwe na wasiwasi.

CCM huwa hamjiongezi , Watu wameanza kuwatoa RAIA wao wiki kadhaa kabla ya Vita hiyo.

Nyie mnastuka saizi tena baada ya Raia kuhoji .

Sasa mipakani tu huko Ukraine, Waafrika wanabaguliwa ,hamna kuondoka , sisi wazungu kwanza ndo tunasepa .
Hatukutarajia kichaa cha Putin kingepanda kiasi hiki....tulidhani ni mikwara tu.
 
Waingie Poland kwa usafiri gani.

Hivi ukimwambia mtu aliyeko mtwara aingie Kenya bila msaada wa kumuwezesha kufika Namanga again ataingia kweli Kenya?

Watawezaje kufika huko na watakuwa wanakula nini?
Serikali ya akina mama. Hii nchi hii
 
Waziri wa Mambo ya nje Mh Mulamula amewataka watanzania takribani 300 walioko Ukraine wajitahidi waweze kuingia Poland ambako uratibu unafanyika.

Mulamula amesema ameona ubaguzi unaoendelea Ukraine kupitia mitandaoni na amesikitishwa sana lakini wananchi wasiwe na wasiwasi kwa sababu serikali inafuatilia kwa karibu sana.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
Very low
Very unconcerned
 
Hili neno' tunafuatilia kwa karibu' huwa silielewi kabisa..
Waafrika tuna shida sana.
Wengine hawa...
Screenshot_20220301-205234_WhatsApp.jpg
 
Kwanini ilishindwa kuwatoa hali ilipoanza kuwa tete wakati wengine walipoanza kuondoka!

Tukumbuke vita haikuanza ghafla kwani maandalizi yalichukua zaidi ya wiki.
... intelejensia ilishindwa kung'amua uwezekano wa vita.
 
Waziri wa Mambo ya nje Mh Mulamula amewataka watanzania takribani 300 walioko Ukraine wajitahidi waweze kuingia Poland ambako uratibu unafanyika.

Mulamula amesema ameona ubaguzi unaoendelea Ukraine kupitia mitandaoni na amesikitishwa sana lakini wananchi wasiwe na wasiwasi kwa sababu serikali inafuatilia kwa karibu sana.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
Wanabaguliwa! Wanaambiwa watembee kwa miguu magari hayatoshi kwa wa'ukraine' wenyewe! Jifunzeni kwa mataifa ya wengine kama China wamewezaje kuwaondoa raia wao zaidi ya 4000!
 
Alichokiongea waziri Mulamula hakina maana wala msaada
Heri angekaa kimya tuu

Mungu wanusuru binadamu wasio na hatia

Mungu watembelee rais wa Russia na Ukraine ukawape moyo wa suluhu badala ya kumwaga damu zisizo na hatia
Angekuwepo Magu haya yasingetokea maana Mulano asingekuwa mambo ya nje na ndege zote za air Tz zingeandamanishwa kwenda kuwachukua watz na WA Africa wanaonyanyapaliwa Ukraine! RIP mwamba raise wetu tuliyekupenda na kutupenda!
 
Back
Top Bottom