Waziri Mwakyembe amemuomba Diamond Platnumz kubadilisha ratiba ya Wasafi Festival mkoani Iringa ili ahudhurie tamasha la JAMAFEST

Waziri Mwakyembe amemuomba Diamond Platnumz kubadilisha ratiba ya Wasafi Festival mkoani Iringa ili ahudhurie tamasha la JAMAFEST

directorpenny

Member
Joined
Jun 18, 2019
Posts
5
Reaction score
3
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amemuomba msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz kubadilisha ratiba ya Wasafi Festival mkoani Iringa ili ahudhurie kwenye tamasha la kizalendo la JAMAFEST.

Akiongea na Waandishi wa Habari Waziri Mwakyembe amesema kuwa tamasha la JAMAFEST (Jumuiya ya Afrika Mashariki Utamaduni Festival) mwaka huu litafanyika katika Uwanja wa Taifa na litadumu kwa siku 8 na litahudhuriwa na wasanii wa ndani na nje ya Tanzania.

Akisisitizia uwepo wa Diamond, Waziri Mwakyembe amesema kuwa “Nimempigia simu kijana wetu nyota wa muziki barani Afrika na pia ulimwenguni ukipenda, Diamond kwamba sasa huu ndio muda wa kuonesha utaifa, hebu njoo ujiunge na sisi. Na atakuwa na ziara siku hiyo mkoani Iringa, Nimemwambia avunje ziara hiyo kwa utaifa, Nafikiri atafanya hivyo. Kwa sababu tulipokuwa Uganda wasanii wote wakubwa nchini humo walihudhuria kwenye tamasha“.

Kwa upande mwingine, Mwakyembe amewaomba Watanzania wahudhurie kwa wingi kwenye tamasha hilo, Wakiwemo wasanii wa Bongo Fleva ili kuonesha uwezo wao.

Tamasha la JAMAFEST litafanyika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania na linatarajiwa kuanza Wikiendi hii Septemba 22 hadi 28, 2019 katika Uwanja wa Taifa.
 
Asante kwa taarifa na mimi nitakuwa hapo kwa ziara rasmi kuangalia washiriki kutoka Rwanda, Burundi na Uganda Wakenya sita watembelea hawana mvuto
 
Itakuwepo na diamond atakuwepo taifa pia
2436b2d04d22792da330526aa43d8524.jpeg
 
Diamond kapost Instagram atakuwepo ila Wasafi Festival Iringa itakuwepo isipokuwa after party ambayo ingekua Jumapili hatakwepocoz baada ya show ataondoka ili kuwahi tamasha/JAMAFEST DAR.
 
Back
Top Bottom