Waziri Mwakyembe asikitishwa na viburi vya TFF, adai kama Amunike ameondolewa basi Karia na wenzie nao wajiuzulu

Waziri Mwakyembe asikitishwa na viburi vya TFF, adai kama Amunike ameondolewa basi Karia na wenzie nao wajiuzulu

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Waziri wa michezo Dr Mwakyembe amesikitishwa na kitendo cha kiburi kilichoonyeshwa na viongozi wa juu wa TFF kwa kushindwa kuhudhuria kikao alichokiitisha.

Dr Mwakyembe amesema aliwaita viongozi wa TFF ili wamueleze sababu za kumfukuza Amunike na kumpa mikakati yao ya baadae lakini viongozi hao wameingia mitini.

Mwakyembe amesisitiza kuwa kama kocha ana matatizo maana yake hata uongozi wa juu wa TFF unapaswa kuwajibika kwa kujiuzulu.
Tarehe 24/07/2019 waziri wa michezo Dr Mwakyembe atakutana na wadau wote wa michezo wakiwemo viongozi wa TFF na hapo atakata mzizi wa fitina na itajulikana maziwa ni yepi na tui la nazi ni lipi, amemalizia.

Source ITV habari

My take;
Mawazo ya Dr Mwakyembe yamefanana na yale yaliyotolewa na Mwenyekiti wa Chadema mzee Mbowe!
 
Wajiuzuru kwa sababu gani? TFF na Mh. Makonda wanapaswa kupongezwa kwa kuifikisha Tz Afcon. Sisi wenyewe tulisema tunaenda kujifunza na sio kushindana. Kuhusu kufukuzwa kocha ni sahihi kabisa maana alikua hana mbinu yoyote. Kuhusu maoni ya Mbowe hayawezi kupewa uzito wowote kwa kuwa ameyatoa kipindi ambacho ana msongo mkubwa wa mawazo ya madeni makubwa anayodaiwa.
 
Hii nchi tatizo sio kocha, hakuna wachezaji.
Hata akija Morinyo, gudiola au fagason bado kipigo kiko pale pale.
 
Wajiuzuru kwa sababu gani? TFF na Mh. Makonda wanapaswa kupongezwa kwa kuifikisha Tz Afcon. Sisi wenyewe tulisema tunaenda kujifunza na sio kushindana. Kuhusu kufukuzwa kocha ni sahihi kabisa maana alikua hana mbinu yoyote. Kuhusu maoni ya Mbowe hayawezi kupewa uzito wowote kwa kuwa ameyatoa kipindi ambacho ana msongo mkubwa wa mawazo ya madeni makubwa anayodaiwa.
Afcon sawa lakini si kufungwa na Kenya. Team ambayo tuna uzoefu wa kuifunga toka enzi za gossage.
 
Huyu maembe nae asitake watu wamnyenyekee kama mungu.timu inaenda kambini hata posho hawajalipwa halafu utegemee ushindi? Imemshinda nae angejiuzulu tu
 
serikali isiingilie soka, tutakula kibano cha FIFA tukiendelea
 
Msema ukweli mpenzi wa Mungu.

Jamaa hana mwonekano wa kimichezo.

Hafai kuwa waziri wa Michezo.

Watenge liwizara abaki huko kwenye Habari n.k. tuwe na wizara ya michezo yenye waziri mwanamichezo. Huyu wamrudishe huko kwenye sheria
 
Back
Top Bottom