Waziri Mwakyembe asikitishwa na viburi vya TFF, adai kama Amunike ameondolewa basi Karia na wenzie nao wajiuzulu

Waziri Mwakyembe asikitishwa na viburi vya TFF, adai kama Amunike ameondolewa basi Karia na wenzie nao wajiuzulu

Kama Waziri haoni mapungufu ya Amunike na anataka viongozi wa TFF nao wang'oke, basi yeye na naibu wake na wao pia waondoke tu sasa
 
Kama Waziri haoni mapungufu ya Amunike na anataka viongozi wa TFF nao wang'oke, basi yeye na naibu wake na wao pia waondoke tu sasa
Karia anayeshughulika na soka 24/7/30/365 ndiye anayepaswa kujiuzulu.

Dr Mwakyembe ana mambo mengi......Habari, Sanaa, Utamaduni na michezo!
 
Waziri wa michezo Dr Mwakyembe amesikitishwa na kitendo cha kiburi kilichoonyeshwa na viongozi wa juu wa TFF kwa kushindwa kuhudhuria kikao alichokiitisha.

Dr Mwakyembe amesema aliwaita viongozi wa TFF ili wamueleze sababu za kumfukuza Amunike na kumpa mikakati yao ya baadae lakini viongozi hao wameingia mitini.

Mwakyembe amesisitiza kuwa kama kocha ana matatizo maana yake hata uongozi wa juu wa TFF unapaswa kuwajibika kwa kujiuzulu.
Tarehe 24/07/2019 waziri wa michezo Dr Mwakyembe atakutana na wadau wote wa michezo wakiwemo viongozi wa TFF na hapo atakata mzizi wa fitina na itajulikana maziwa ni yepi na tui la nazi ni lipi, amemalizia.

Source ITV habari

My take;
Mawazo ya Dr Mwakyembe yamefanana na yale yaliyotolewa na Mwenyekiti wa Chadema mzee Mbowe!
Amunke alistahili kuondoka baada ya mechi za kufuzu AFCON 2019. Wala sio tatizo la uongozi wa TFF. Ikumbukwe kuwa kufungwa kwa Taifa Stars siyo sababu ya kuondolewa kwake. Bali mfumo wake wa kuingoza timu na kupanga kikosi na kufanya mabadiliko kulionyesha kuwa ama anaihujumu au hajui.
 
Wewe umesomea wapi ukocha?!
 
Back
Top Bottom