Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba amezungumzia kuhusu Mjadala wa Dola kuadimika unaoendelea Nchi.
Amesema watu inabidi watambue kwamba Dola sio hela yetu bali tunaipata pale tunapopata Mkopo, Msaada, tunapouza bidhaa ama Huduma nje ya Nchi ndo tunapata Dola.
Sera za kifedha za Marekani kukabiliwa na mfumuko wa bei fedha wamezirudisha fedha ndani ya Central Bank yao Marekani.
Sababu za ndani zinazofanya dola ziadimike ni Matumizi. Matumizi yake yamekuwa makubwa.
Mitambo tunayojengea Bwawa la Mwalimu Nyerere vinanunuliwa kwa Dola, Ujenzi wa Reli Mitambo yake vinanunuliwa kwa Dola, Mikopo yetu tunalipa kwa Dola.
Kwahiyo Dola inatumika sana kuliko vitu vinavyotuletea Dola.
Wafanyabiashara wa hapa, wanapopeleka bidhaa nchi za jirani hawapewi dola. Kwa sasa Sisi tuna Dola Bil 5.2 kuwazidi wenzetu.
Ukame wa dola upo pote. Hii akiba hatuitoi sababu ndo tunalipia deni ili tusije tangazwa tumefilisika
Til 11 tunalipa kwa Mwaka deni la Taifa.
Watu wanadhani ni kazi ya benki kuu kutoa dola. Dola wanapatiana kwenye soko. Mara ya mwisho Benki kuu imetoa dola 2012 hadi 2022 baada ya Uviko. Baada ya Uviko Ilikuwa inatoa Mil 500.. Kwa Sasa tunatoa Milioni 10 na bado haitoshi sababu uhitaji ni mkubwa kila sehemu.
Majibu ya Mwigulu kuhusu dola kuadimika,
1. Dola sio hela yetu.
2. Marekani wamezirudisha kwenye central bank.
3. Matumizi yake ya ndani yamekuwa makubwa ndio maana zimeadimika.
4. Mitambo tunanunua kwa dola.
5. Mikopo yetu tunalipa kwa dola.
6. Wafanyabiashara wakiuza nje hawapewi dola.
Yaani hawa jamaa wameshaachana..ila muda utaendelea kusema.
Walivamia nchi kwa mbwembwe na mashauzi..wakataka kupendwa na kuonekana wao wazuri..wakataka kufurahisha kundi la wachache. Sasa wamebaki peke yao..wanazidi kuadhirika..sasa wanatafutana kila kona. Mugambo wanaruka na kukanyagana.
Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba amezungumzia kuhusu Mjadala wa Dola kuadimika unaoendelea Nchi.
Amesema watu inabidi watambue kwamba Dola sio hela yetu bali tunaipata pale tunapopata Mkopo, tunapouza bidhaa ama Huduma nje ya Nchi ndo tunapata Dola...
Kwani hatujuwi dola siyo yetu?! The guy is a twat and a prick!
Kuna vijiswali vidogo..
Royal Tour kumbe ilikuwa maigizo?
Alizoacha JPM mnadai zimelipa madeni au?
Madini, Tanzanite, Gold, etc etc hela zimeenda wapi?
Tuliwaasa muache mbwembwe za kusafiri, kununuwa ma V8, na ujinga mwingi wa kutumia hela kama vile tunazo, mkakataa kubana matumizi na kujifanya mama kafunguwa maakaunti na nchi mko wapi Sasa?
Sas si tuliambiwa mauzo ya nje yameongezeka?
Si tuliambiwa watalii wameongezeka?
Si tuliambiwa dola zimemwagika kutokana na watalii na utalii kuongezeka kwa kasi kutokana na royal tour?
Kwa hiyo sababu ya hela kupotea inatokana na kutoiprint? Kwa hiyo ingekuwa yetu tungeprint tuu?
Kwani ujenzi wa bwawa la umeme na hayo yote yameanza mwaka huu?
Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba amezungumzia kuhusu Mjadala wa Dola kuadimika unaoendelea Nchi.
Amesema watu inabidi watambue kwamba Dola sio hela yetu bali tunaipata pale tunapopata Mkopo, Msaada, tunapouza bidhaa ama Huduma nje ya Nchi ndo tunapata Dola...
Waziri mwenyewe wa fedha hana ubunifu. Wenzake wanajipeleka karibu na brics kununua mafuta kwa hela zao urusi.
Kuna fursa ya kufanya biashara bila dola na mataifa kama Uchina India Urusi ila wanajikita kwenye mfumo chakavu wa kinyonyaji wa kutegemea dola maana vigogo ni wajinga au wana maslahi.
Nakumbuka wakati nasafiri mwaka 1977 tulichenji hiyo $ kwa sh 12 na tulipewa $1000 tu na ikaandikwa kwenye passport
Wakati huo kulikuwa na waadilifu asiwaambie mtu