Waziri Mwigulu: Kutoza ndani ya nchi kwa dola ni kosa, watakiwa kuacha kuanzia Julai mosi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mwigulu Nchemba akisoma bajeti ya serikali bungeni amesema suala la taasisi binfasi na za umma kutaka malipo ya huduma kwa fedha za kigeni zinaleta shida kwa watanzania kwa kuwa wanatumia Tsh na sio dola.

Amesema suala hili linafanya watanzania kuhangaika kuipata dola, wakati inabidi hata wageni wakija nchini wahangaike kuipata shilingi na sio dola. Kutokana na jambo hilo amesema kuwa kuanzia Julai 1, 2024 malipo yote kwa taasisi za umma na binafsi watatakiwa kupokea malipo kwa shilingi tu.

Aidha amesema kama mtu atakuja na fedha za kigeni, atatakiwa kwanza kuzibadilisha na kupata shilingi ya Tanzania ili kufanya malipo

===

Pia soma:
- News Alert: - Waziri Mwigulu awasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025
 
Mwigulu ameongelea watanzania kulikuza tatizo la upungufu wa dola kudai au kufanya malipo ya bidhaa na huduma zinazotolewa ndani ya nchi kwa kutumia fedha ya kigeni. Mwigulu amesema kulipa kwa fedha za kigeni nchini kunaifanya shilingi ikose thamani na dola kuwa na thamani ndani ya nchi.

Mwigulu amesema kuuza bidhaa au huduma kwa kutumia fedha za kigeni ni kosa kwa mujibu wa kifungu cha 26 cha sheria ya benki kuu ya mwaka 2006 ambacho kinabainisha shilingi ya Tanzania ndio fedha pekee ya malipo ndani ya nchi.

Mwigulu amehimiza wananchi na wadau kuacha kulipa au kununua vitu kwa fedha za kigeni kwani ni haki kisheria kwa kutumia sarafu ya shilingi.

Mwigulu ameielekeza benki kuu na vyombo vingine kuratibu jambo hilo kwa ufanisi.

Hatua nzuri lakini nimkumbushe Mwigulu kuna baadhi ya taasisi za Serikali zinadai malipo ya fedha za kigeni hasa kwa wageni na ni hitaji la lazima.
 
Mwigulu ameongelea kulipa kwa fedha za kigeni nchini kunaifanya shilingi ikose thamani na dola kuwa na thamani ndani ya nchi.

Mwigulu amehimiza wananchi na wadau kuacha kulipa au kununua vitu kwa fedha za kigeni
Nimeamini huyu jama hajui uchumi sababu sio hiyo sababu ni shilling yetu haina stability na nguvu, eti ana phd ya uchuumi loh.
 
Mwigulu Nchemba akisoma bajeti ya serikali bungeni amesema suala la taasisi binfasi na za umma kutaka malipo ya huduma kwa fedha za kigeni zinaleta shida kwa watanzania kwa kuwa wanatumia Tsh na sio dola...
Mkumbushe kwamba Tanzania ni free market economy, impangie mwenye pesa jinsi ya kutumia au kupokea pesa yake, asiturudishe kwenye command economy.
 
Nahisi kuwa kama itakuwa hivyo basi vibali vya kununua na kuuza dola viko njiani.Enzi zileee
 
Gari la milioni sita linapiwa kodi milioni 16 kwa sababu ya usd upo sahihi kama utafanikisha itakua jambo jema maana ni Tanzania pekee ndio tuna malipo ya usd kwenye taasisi za Umma..
 
Mkuu hilo sahau wanachangamsha genge tu, wanajua pesa yetu inaporomoka lazima wanapanga kodi kutumia US dolar.
 
Najua mkuu maana jamaa kila akiamka anaongea anachotaka na anajua hata kisipotekelezwa afanywi kitu..
 
Mwigulu Nchemba akisoma bajeti ya serikali bungeni amesema suala la taasisi binfasi na za umma kutaka malipo ya huduma kwa fedha za kigeni zinaleta shida kwa watanzania kwa kuwa wanatumia Tsh na sio dola.

Amesema suala hili linafanya watanzania kuhangaika kuipata dola, wakati inabidi hata wageni wakija nchini wahangaike kuipata shilingi na sio dola. Kutokana na jambo hilo amesema kuwa kuanzia Julai 1, 2024 malipo yote kwa taasisi za umma na binafsi watatakiwa kupokea malipo kwa shilingi tu.

Aidha amesema kama mtu atakuja na fedha za kigeni, atatakiwa kwanza kuzibadilisha na kupata shilingi ya Tanzania ili kufanya malipo
huyu jamaa hili nalo atakwama kutokana na hali halisi hana maono
 
Mwigulu Nchemba akisoma bajeti ya serikali bungeni amesema suala la taasisi binfasi na za umma kutaka malipo ya huduma kwa fedha za kigeni zinaleta shida kwa watanzania kwa kuwa wanatumia Tsh na sio dola.

Amesema suala hili linafanya watanzania kuhangaika kuipata dola, wakati inabidi hata wageni wakija nchini wahangaike kuipata shilingi na sio dola. Kutokana na jambo hilo amesema kuwa kuanzia Julai 1, 2024 malipo yote kwa taasisi za umma na binafsi watatakiwa kupokea malipo kwa shilingi tu.

Aidha amesema kama mtu atakuja na fedha za kigeni, atatakiwa kwanza kuzibadilisha na kupata shilingi ya Tanzania ili kufanya malipo
Kwani hao TANAPA na Tanroads kwenye fine na tozo walianza leo kutoza kwa dola? Kuna shida sehemu Mwingulu anatakiwa kwenda kupewa shule lakini hii sio sababu maana dola kuadimika ni shida kuanzia mwaka jana…
 
tunaogopa kukaa na TSH maana hatuoni juhudi zozote zakuifanya iwe strong zaidi ya blahblah za kitoto tu.

Bora tutunze ndani Mnyamwezi $ au malkia £, ambazo baada ya 5yrs unazungumzia faida sio hasara.

Tuanze kwanza kuifanya TSH strong.
 
Nimeamini huyu jama hajui uchumi sababu sio hiyo sababu ni shilling yetu haina stability na nguvu, eti ana phd ya uchuumi loh.
Unashauri afanye nini? Naona unalalamika tu haitoi ushauri nini afanye
 
Back
Top Bottom