johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Waziri wa fedha Dr Mwigulu Nchemba amesema mfumuko wa bei unaolalamikiwa hausababishwi na sera zetu wala uzembe.
Kadhalika, fedha ya mkopo wa COVID 19 kutoka IMF imesaidia kuongeza mzunguko wa fedha mitaani na hasa katika maeneo yote ya vijijini ambako fedha hizi bado zinazunguka.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha amesema deni la taifa ni himilivu na mambo yanaenda kama yalivyopangwa.
===
Waziri wa Fedha na Mipango Mh. Dkt. Mwigulu Nchemba amesema mfumuko wa bei na kupanda kwa gharama za maisha kwa wananchi hakusababishwi na tatizo la kisera wala uzembe bali unatokana na uwepo wa majanga yanayoendelea kuikumba dunia.
Dkt. Mwigulu ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wahariri wa vyombo vya Habari akieleza utendaji na mafanikio ya serikali ya awamu ya sita katika kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Chanzo: ITV habari