Waziri Mwigulu Nechemba aishukuru Italia kwa kuipa mkopo Tanzania kujenga SGR

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,536
Reaction score
7,194
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba ameishukuru Italia kwa kutoa dhamana ya mkopo wa kujenga Reli ya Kisasa (SGR), kipande cha Kwanza na cha pili kuanzia Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma hadi Makutupora mkoani Singida, ambavyo ujenzi wake umekamilika na treni imeanza kutoa huduma kuanzia Dar es salaam hadi Dodoma.

Mhe. Dkt. Nchemba ametoa shukrani hizo mjini Rome nchini Italia, alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Italia (SACE), Bi. Alessandra Ricci.

Alieleza kuwa kutokana na mchango huo, SGR imeanza kutoa huduma ya kubeba abiria kuanzia Julai mwaka 2024, ikiwa ni mafanikio makubwa katika historia ya usafiri nchini, ambapo muda wa safari kati ya Dar es Salaam na Dodoma umepungua kutoka saa nane hadi takriban saa tatu.

Aidha, Mhe. Waziri Nchemba alieleza kuwa Serikali inatambua na kuthamini nia njema ya SACE kuendelea kudhamini ujenzi wa reli toka Dodoma hadi Isaka

Aidha, Dkt. Nchemba aliwaalika wawekezaji kutoka Italia kwenda kuwekeza nchini Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo uendeshaji wa miundombinu ya reli pamoja na ujenzi wa viwanda vitakavyosaidia kukuza ajira na kukuza uchumi wa nchi wa pande hizo mbili.

Snapins.ai_488315355_455150737622163_2878214723638760352_n_1080.jpg

Snapins.ai_487942966_3450716821726121_1254677414380741409_n_1080.jpg

Source: Manara TV
 
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba ameishukuru Italia kwa kutoa dhamana ya mkopo wa kujenga Reli ya Kisasa (SGR), kipande cha Kwanza na cha pili kuanzia Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma hadi Makutupora mkoani Singida, ambavyo ujenzi wake umekamilika na treni imeanza kutoa huduma kuanzia Dar es salaam hadi Dodoma.

Mhe. Dkt. Nchemba ametoa shukrani hizo mjini Rome nchini Italia, alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Italia (SACE), Bi. Alessandra Ricci.

Alieleza kuwa kutokana na mchango huo, SGR imeanza kutoa huduma ya kubeba abiria kuanzia Julai mwaka 2024, ikiwa ni mafanikio makubwa katika historia ya usafiri nchini, ambapo muda wa safari kati ya Dar es Salaam na Dodoma umepungua kutoka saa nane hadi takriban saa tatu.

Aidha, Mhe. Waziri Nchemba alieleza kuwa Serikali inatambua na kuthamini nia njema ya SACE kuendelea kudhamini ujenzi wa reli toka Dodoma hadi Isaka

Aidha, Dkt. Nchemba aliwaalika wawekezaji kutoka Italia kwenda kuwekeza nchini Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo uendeshaji wa miundombinu ya reli pamoja na ujenzi wa viwanda vitakavyosaidia kukuza ajira na kukuza uchumi wa nchi wa pande hizo mbili.

Source: Manara TV
Ela zitumike kujenga reli sasa na sio kugawana na kwenda kuhifadhi kwenye mabenki ya njee
 
Mkopo wa kipande cha tano bado hujapatikana?
 
Back
Top Bottom