Waziri Mwigulu: Tunatazamia kuwakopesha Wafanyakazi wenye sifa Magari ili kupunguza Matumizi ya Serikali

Swali na majibu.

Phd vilaza..
 
Kwa nini serikali iwakopeshe?
Hivi hamuelewi pesa ya serikali ni pesa ya wananchi maana ni kodi zao.

Wananchi mmesikia, serikali inakopesha magari so mimi na wewe ni haki yetu pia..

Magari yanakopeshwa na financial institutions sio serikali.
Kila mfanyakazi wa umma awe waziri mbunge Mkuu wa Mkoa wilaya kijiji mtaa wote wanapashwa kugharamia magari yao sio kodi za wananchi. Gari za wizara sijui ni gari za serikali ambapo matumizi ni ya kiserikali sio kwenda nayo nje kwa shughuli binafsi aka kufukuzia demus…

Huyu asitufanye Sisi wajinga.
Wananchi mkuye huku kuna pesa za kukopa magari lakini hakuna pesa ya kujenga barabara huko madaba na kwingineko

Hii nchi ngumu sana mweh!
 
Serikali gari haiuzwi kwa bei ya kununulia.
Inashuka vibaya mno na inaweza kununuliwa kwa bei ya nyanya
Nachomaanisha, wakopeshwaji watakopa magari ya Bei himilivu watakayomudu matengenezo hivyo gharama na matumizi yayapungua.
 
Wataalamu wa manunuzi ya kimataifa hebu mtusaidie sisi ambao hatuna exposure.

Je, ni kweli kuna makampuni hayapendi serikali kwenda kununua mfano magari moja kwa moja kiwandani? Kwa mfano, serikali inaenda TOYOTA Japani na kusema tunataka magari 200, halafu hao Toyota wanasema, rudini Tanzania mkaonane na wakala wetu! wakati huo huo wanajua kwamba hawapo peke yao wanaozalisha magari!

Vipi kwenye ununuzi wa ndege napo kuna mawakala wanatumika?
 
Ukisoma btn the lines.

V8 zitabaki Kwa Rais na Pm bas, wengine watarudi kwenye Land cruiser mkonga.

Na kinachosikitisha, wanachukua hatua hizo Leo, Si kwamba wanasikiza wananchi no, ni kwamba madeni yamewaelemea.
Land cruizer mkonga mpya bei gani?
Salary 3-4M kabla ya makato italipa hiyo gari kwa muda gani?
 
Ni malengo makubwa lakini waziri wa uchumi alitakiwa awe anawaza ni namna gani tutaunda magari hapa nyumbani.
 
Mwigulu ni waziri wa fedha mbumbumbu haijawahi kutokea!! Huko nyuma utaratibu huu uliwahi kutumika na makusudio ya kupunguza matumizi ya magari kwa viongozi na maofisa hayakufanikiwa kwasababu ya usimamizi mbovu; walikopeshwa magari wakayapaki Nyumbani na kuendelea kutumia magari ya pool!!
Tatizo ya serikali ni jinsi ya kuthibiti matumizi yake. Huwezi kufanikiwa iwapo waziri wa fedha ni kilaza ; huyu huyu waziri anasema hadharani kuwa hakuna wizi wa fedha za serikali wakati report ya CAG inaeleza kwa unfamiliar jinsi wizi wa fedha za serikali ulivyo shamiri nchini!
Ni waziri wa fedha ambaye hata hajui athari ya nchi kuwa na deni la Taifa lisiloweza kubebeka kwani kwake kukopa kopa nchi za nje ndio suluhisho la matatizo ya nchi!
Kuwa na viongozi wa namna hii ni kulipeleka Taifa jehanam.
 
Na mafuta na matengenezo mtupe Pua
 
Sasa gari ya milioni mia tatu huyo DED au DC atamaliza lini kulilipa?? AU atakuwa kwenye ajira only kununua gari?
Kumbe haujui janja yao!! Gari la milioni 300 anauziwa kwa mkopo mfanyakazi kwa sh milioni 30 tu!! Halafu anapewa malipo ya milage kila mwezi!!
 
Swali la msingi lilikuwa "kwanini tunanunua Kwa bei kubwa kuliko kwenye soko la dunia"
Sijaona kama swali limejibiwa
 
Magari ya Watumishi wa Serikali wanaostahili kukopeshwa Lazima yatakuwa na Bei ya chini kutokana na ukweli magari hayo yanauzwa na Serikali yenyewe

Pili, Magari hayo yatatumiwa na Watumishi kwenye Shughuli za kila siku za Serikali

Sidhani kama Magari hayo yana kodi

Hivyo usidhani V8 ya tsh 400mil na mkopo wake utasomeka hivyo, yawezekana kabisa ikawa chini ya tsh 50mil

Jumaa Mubarak 😀
 
Umeandika nini hiki mzee mgaya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…