Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Waziri wa Habari, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Nape Nnauye amesema wanaona mijadala yote inayoendelea (kuhusu maoni ya kama mtandao wa X ufungiwe au laah) na kusema Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), itatimiza wajibu wake wa kuhakikisha Tanzania na hususani kizazi cha Watoto kipo salama.
Pia soma: CCM na Serikali tuambieni ukweli, kelele za kutaka X(Twitter) ifungiwe ni maandalizi ya kuzima mitandao kipindi cha uchaguzi
Akijibu hoja za Wadau kwenye mtandao wa X, Nape amesema “TCRA watapima madhara yatokanayo na mabadiliko ya sera yaliyofanywa na mtandao husika (X zamani Twitter) na mitando mingine na kuchukua hatua stahiki kwa wakati sahihi”