Waziri Nape ashangaa masuala ya mifumo nchini kutosomana

Waziri Nape ameyasema hayo katika Kongamano la Jukwaa la Fikra kuhusu mabadiliko ya digitali leo tar 20 jijini Dar, akisema kuwa inauma kusikia mifumo ya Tanzania bado haiwezi kusomana.

Ametolea mfano kipindi alipoenda Hospitali ya Benjamin Mkapa na kufanya kipimo cha MRI ya mguu wake halafu alivyoenda Muhimbili MOI hawakuweza kupata taarifa hiyo na kumwambia afanye kipimo tena.

Kama waziri anashangazwa na kuumia, sisi wengine tufanye nini?

Anaelewa nini kuhusu programming na softwares? Lazima ashangae kama ni mashikolo mageni. Zumaridi alishangaa minara ya Gamboshi alikuwa hajawahi kufika😂😂😂😂
 
Huu msamiati mpya "kusomana" utatumika sana kupigia pesa!
 
Waziri Nape ameyasema hayo katika Kongamano la Jukwaa la Fikra kuhusu mabadiliko ya digitali leo tar 20 jijini Dar, akisema kuwa inauma kusikia mifumo ya Tanzania bado haiwezi kusomana.

Ametolea mfano kipindi alipoenda Hospitali ya Benjamin Mkapa na kufanya kipimo cha MRI ya mguu wake halafu alivyoenda Muhimbili MOI hawakuweza kupata taarifa hiyo na kumwambia afanye kipimo tena.

Kama waziri anashangazwa na kuumia, sisi wengine tufanye nini?
Isingekuwa inasoma tungeionaje hii.
FB_IMG_1681189841254.jpg
 
Back
Top Bottom