Waziri Nape, kuna dosari kwenye zoezi la anuani za Mitaa

Waziri Nape, kuna dosari kwenye zoezi la anuani za Mitaa

HEKIMA KWANZA

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2015
Posts
2,942
Reaction score
3,937
Waziri Nape, kuna dosari kwenye zoezi la anuani za Mitaa. Ipo mitaa inandikwa kwa jina la Kiswahili na mingine inaandikwa kwa lugha ya Kiingereza.

Unakute vibao viwili vinavyotumia mlingoti mmoja, kimoja kimeandika Mtaa wa MTAA WA MARKET, na kibao kingine kwenye mlingoti huo huo kimeandikwa UHURU ROAD! Nakushauri uteremke kwenye hiyo helikopta ili uone kasoro zinazoendelea huku ardhini.

Mitaa mingine unakuta imeandiki MAPINDUZI LOAD! Nchi inaonekana haiko makini kabisa na wewe Waziri unaonekana huna mkakati wa kueleweka wa kusimamia hili zoezi. Kaa na watu wako mrekebishe hayo makosa, ni aibu.

Wengine mnaweza kuongeza dosari mnazoziona kwenye maeneo yenu.
 
Sina uhakika kama wanaofanya hiyo kazi wanalipwa.

Mbongo usipomlipa atakufanyia kazi vizuri tu na kwa wakati. Ila utajuta.
 
Back
Top Bottom