Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Makampuni mengi ya kitanzania hayana mfumo wa ku fact check, na hata yanayofanya hivyo hutumia kampuni za nje ambazo hata kiswahili chao siyo kizuri.
Unaweza kukuta mtu kaandika Nape kaumwa wakati siyo kweli. Nafarijika kuona jambo hili limezinduliwa leo na ndiyo maana nipo hapa. Kama serikali tungetamani kupata ukweli wa taarifa hivyo Nawashukuru Jamii Forums kuwa kusaidia jambo hili.
Uzuri ni kuwa jukwaa hili halijaanzishwa na Serikali, nina furaha sasa kuwa facts zitakuwa checked, na niwahakikishie kuwa Serikali tutawaunga mkono.
Mnaenda kuufanya mtandao kuwa salama, sasa ni kazi ya wizara yangu kuhakikisha upande wa cyber tupo vizuri.
Mimi pia ni mwanachama, natukanwa sana, nina ngozi ngumu, mara nyingi huwa naingia huko ninapokuwa nimechoka.
Katika mazingira ya kidigitali, mtu yeyote anaweza kuandaa chochote na kukisambaza mtandaoni, ni bahati mbaya majukwaa yanayopokea stori nyingi na wanatumia hizo taarifa bila kuhakiki
Bahati mbaya wale wa nje tena wengine ambao hawajui hata Kiswahili vizuri wanatumia taarifa hizo kama zilivyo
Nimekuja hapa ni kwa kuwa Tanzania tuna ‘fact check’ ambayo inaweza kuhakiki taarifa na kupata ukweli, ninafurahi kwamba ‘Fact Check’ ni ya jamii, ingekuwa ni ya Serikali wangesema labda kuna kitu tunafanya
Wito wangu, hasa kwa majukwaa ya kimataifa, wafanye makubaliano na Jamii Forums kupata uhakika wa kile kinachoandikwa na kutokea, badala ya kuendeleza upotoshaji
Jamii Forums imesaidia kazi ya Wizara yangu, kupata sehemu ambapo kutakuwa na uhakika wa kupata taarifa za ukweli,
Niwathibktishie kama Serikali tutawapa ushirikiano, kazi mnatofanya ni ya kizalendo na mnasaidia Serikali
Kwa niaba ya Serikali, mnafanya kazi nzuri ya kulinda taswira ya TZ, likitumika vizuri siyo tu jamii yetu, bali dunia itapata sehemu ya kupata ukweli
Mnachangia mtandao kuwa salama, ni kazi ya Wizara yangu kuhakikisha mtandao unakuwa salama, nawapongeza sana
Nimekuwa mwanachama, nasoma mambo mengi, wakati mwingine natukanwa humo ndani, lakini mnafanya kazi nzuri
Nitoe rai kwa wote mliopo hapa, tuisaidie jamii kuwa na chachu ya kupata yaliyo mema,tuwajengee wananchi kubishana kwa hoja
Shindano hili la Stories of Changes (SOC) tangu lianze limeibua mambo mengi ya msingi na hivyo ndivyo inavyotakiwa
Tangu Rais Samia alivyoingia madarakani hatusikii watu wakifinywafinywa, wewe sema sisi tutapima, la maana tutabeba, ambalo tutaona ni la hasira tu tutaliacha
Ninaahidi kuwa nanyi bega kwa bega, kuendeleza kulinda Sheria za muongozi ikiwemo Muswada wa Sheria ya Ulinzi Binafsi, pia nichukue nafasi hii kuwapongeza #JamiiForums kuhakikisha sheria hii inapita, wamenitia moyo sana, jambo hili lilishindikana kwa miaka 9.
Natambua mchango huu wa #JamiiForums na wadau wengine walioungana katika kuhakikisha Muswada Sheria ya Ulinzi Binafsi inapatikana
Niwahikikishie wadau kuwa mchakato upo sehemu nzuri, nina hakika Wabunge watatusaidia katika kuhakikisha unafanikiwa na kuwa Sheria