Waziri Nape Nnauye aitaka TCRA kuyaagiza Makampuni ya Mawasiliano kusitisha upandishaji wa bei ya Vifurushi

Waziri Nape Nnauye aitaka TCRA kuyaagiza Makampuni ya Mawasiliano kusitisha upandishaji wa bei ya Vifurushi

tena walichinja vifurushi kimya kimya na sisi tukakosa pa kuanzia ...

matamko mazuri mashaAllah ila utekelezahi sasa ?

yule wa vifaa vya ujenzi na vinywaji sioni kinachofanyika maana hata leo nimenunua nondo sh.elfu 27 na wakati walipewa siku tatu ...
Haya mabando yamepanda lini?
 
Waziri wa Habari na Teknolojia ya Habari Mhe Nape Nnauye ameiagiza TCRA kuyaagiza makampuni ya simu kusitisha upandishaji wa bei ya Vifurushi mpaka hapo watakapokaa na Serikali kuzungumza kuhusu jambo hilo.

Chanzo: DarMpya

Pia soma
- Gharama za vifurushi vya intaneti zapandishwa tena kimya kimya. Je, ni censorship ya aina yake?
View attachment 2090532

Waziri wa Habari na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye​
Maigizo tupu hata Ndugulile aliagiza lakini matokeo yake yakawa tofauti kabisa
 
tena walichinja vifurushi kimya kimya na sisi tukakosa pa kuanzia ...

matamko mazuri mashaAllah ila utekelezahi sasa ?

yule wa vifaa vya ujenzi na vinywaji sioni kinachofanyika maana hata leo nimenunua nondo sh.elfu 27 na wakati walipewa siku tatu ...
Sasahivi kuna matamko tupu lakini utekelezaji ni zero kabisa
 
Tatizo lipo kwa Waziri wa Fedha, jamaa gaidi sana yule.
 
Ni marudio tu, makampuni ni mali yao wao wanaohoji.
Siasa tu hiyo, hakuna kitu. Wamiliki ni wakubwa hao hao. Nani asiye jua hela ya serikali ilivyo pindishwa toka ttcl kuanzishwa AIRTEL? Mkopo toka world bank ulivyo pindishwa kuingia mikono binafsi na kuanzishwa halotel? Anatafuta mgao wake.
 
Hawezi kuingilia huko. Yeye anacheza na vitu viko chini ya wizara take.
Yeye amezungumzia serikali , ina maana serikali nzima inaundwa na nape tu?kama wana huruma hiyo hao mawaziri wa wizara nyingine, wako wapi?juzi waziri anataka maelezo eti kwanini soda zimepanda bei?!!
 
Dogo katika ubora wake.
Juzi juzi aliahidi ndani ya miezi mitano kila nyumba itakua na physical address.
Juzi Kati katoa agizo kila muandishi aliyekufa alipwe ndani ya wiki mbili.
Leo Tena.
 
Hayo mambo ya vitabuni, kwa sasa karibu makampuni yote bei zinafanana na zimepandishwa na serikali wala si makampuni.

Nilikuwa nanunua gb. 7 halotel kwa 5000 tu sasa hivi kwa 10000 ndio napata hizo gb 7, Ni wizi wa mchana.
Hiki ni kifurushi gani maana kwangu hata 10,000 napata GB 4.9 tu
 
Back
Top Bottom