Waziri Nape Nnauye aonya wanaohamasisha ushoga kupitia WhatsApp

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
6,404
Reaction score
6,969
Waziri wa Habari Nape Nnauye ametoa onyo kwa viongozi wa makundi ya WhatsApp (Admin), wazazi na wanaohusika kusambaza mitandaoni jumbe na video zinazohamasisha vitendo vya usagaji na ushoga na wengine wakitumia maudhui kwa njia ya cartoon ambazo hupendwa na watoto.

----
Serikali imetangaza kuanza kuchukua hatua kali kwa watu watakaobainika kusambaza maudhui yanayohamasisha mapenzi ya jinsi moja.

Pia, amewatahadharisha viongozi wa makundi ya ya WhatsApp ma ‘admin’ ambao hawatafuata au kuchukua hatua kwa wanaosambaza maudhui ya mapenzi ya jinsi moja yakiambatanishwa na video au picha kuwa watachukuliwa hatua kali pamoja na vyombo vya habari.

Hayo yamesemwa leo Jumapili Septemba 11, 2022 na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye jijini Dar es Salaam.

Amesema hatua hiyo imekuja kufuatia kukithiri kwa vipande vya video zinazosambaa mitandaoni zikionyesha vitendo vya aina hiyo.

Waziri Nape amesema kuanzia sasa Serikali haitavumilia kuendelea kusambaa kwa maudhui hayo na itafanya hivyo kwa wote wanaosambaza hata kama wanafanya hivyo kwa lengo la kutahadharisha.

“Tumeendelea kufuatilia anga la mtandao wetu, liko salama isipokuwa hizi changamoto ndogo ndogo na hivi karibuni tunaona kumekuwa na usambaaji wa video zinazohamasisha ushoga na usagaji.

“Tumefuatilia kwenye vyombo vyetu ambavyo tumevipa leseni hakuna ambacho kinahusika katika hili, watu wanapakua kupitia pay tv matokeo yake zinasambaa kupitia mitandao ya kijamii hasa makundi ya WhatsApp,”amesema Nape na kuongeza.

“Sasa nitoe tahadhari tutakapoanza kuwazoa, hatutegemei taharuki maana hadi mimi kujitokeza kuzungumzia hili suala ni wazi kwamba tumeamua kulifanyia kazi. Kuweni makini huko kwenye mitandao na makundi ya WhatsApp hasa ma admin hatuna utani katika hili,” amesema .

Chanzo: Mwananchi
 
Hayo ni mawazo yake binafsi sio msimamo wa serikali maana serikali isha toa muongozo kitambo Sana [emoji116]
JamiiForums1269281912.jpg

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hahahahaha unahitaji kuacha kuwa mnafiki katika hili ili kulimaliza au kuliondoa.

Iwekwe tu kwenye sheria ya nchi marufuku ushoga Tanzania, ukigundulika adhabu ni kufa.

Lingine la msingi ni kusisitiza na kusimamia maadili kuanza shule za msingi, sekondari na vyuo vikuu, watu wa ustawi wa jamii wamelala maofisini huku Taifa likiangamia kimaadili.

Viongozi mmeacha majukumu yenu ya kwa jamii yote nanyie mmejikita kwenye familia zenu ilihali ni viongozi wa umma.
 
Waziri wa Habari Nape Nnauye ametoa onyo kwa viongozi wa makundi ya WhatsApp (Admin), wazazi na wanaohusika kusambaza mitandaoni jumbe na video zinazohamasisha vitendo vya usagaji na ushoga na wengine wakitumia maudhui kwa njia ya cartoon ambazo hupendwa na watoto.

----
Serikali imetangaza kuanza kuchukua hatua kali kwa watu watakaobainika kusambaza maudhui yanayohamasisha mapenzi ya jinsi moja.

Pia, amewatahadharisha viongozi wa makundi ya ya WhatsApp ma ‘admin’ ambao hawatafuata au kuchukua hatua kwa wanaosambaza maudhui ya mapenzi ya jinsi moja yakiambatanishwa na video au picha kuwa watachukuliwa hatua kali pamoja na vyombo vya habari.

Hayo yamesemwa leo Jumapili Septemba 11, 2022 na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye jijini Dar es Salaam.

Amesema hatua hiyo imekuja kufuatia kukithiri kwa vipande vya video zinazosambaa mitandaoni zikionyesha vitendo vya aina hiyo.

Waziri Nape amesema kuanzia sasa Serikali haitavumilia kuendelea kusambaa kwa maudhui hayo na itafanya hivyo kwa wote wanaosambaza hata kama wanafanya hivyo kwa lengo la kutahadharisha.

“Tumeendelea kufuatilia anga la mtandao wetu, liko salama isipokuwa hizi changamoto ndogo ndogo na hivi karibuni tunaona kumekuwa na usambaaji wa video zinazohamasisha ushoga na usagaji.

“Tumefuatilia kwenye vyombo vyetu ambavyo tumevipa leseni hakuna ambacho kinahusika katika hili, watu wanapakua kupitia pay tv matokeo yake zinasambaa kupitia mitandao ya kijamii hasa makundi ya WhatsApp,”amesema Nape na kuongeza.

“Sasa nitoe tahadhari tutakapoanza kuwazoa, hatutegemei taharuki maana hadi mimi kujitokeza kuzungumzia hili suala ni wazi kwamba tumeamua kulifanyia kazi. Kuweni makini huko kwenye mitandao na makundi ya WhatsApp hasa ma admin hatuna utani katika hili,” amesema .

Chanzo: Mwananchi
Huu uongo umewekwa hapa kuziba ukweli wote! Hili lijamaa lilitaka kuzuia matumizi ya mitandao kwa ujumla tu!
 
Mimi naona hio sio issue ya msingi ya kutusahaulisha mfumuko wa bei ya kila kitu maana mtu kama anaamua kutoa mk..ndu wake sasa mimi naathirika na nini?
 
Oyoo waziri hebu tuambie kwa nini unatumia gari la kifahari kwa kodi zetu ?

Hilo la mashoga na wasagaji muachie Mungu awapige kibiriti hao wahuni, we huwawezi hao acha mkwara mbuzi

Uwezacho ni kukataa kutumia gari la kifahari ili kodi zetu zitumike kwa manufaa ya wananchi. Usiseme hatujakushauri.
 
Back
Top Bottom